Ticker

    Loading......

VISIGA SEKONDARI IFUNGULIWE MAPEMA TUWAPUNGUZIE WANAFUNZI UMBALI WA KUTEMBEA -DKT JAFO

 Na Didas Olang, Kisarawe-Pwani.

Mbunge wa Jimbo la Kisarawe Dkt Selemani Said Jafo ambaye pia ni Waziri wa Viwanda na Biashara amemuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya kisarawe kuharakisha Ujenzi wa Miundombinu saidizi katika shule mpya ya Sekondari Visiga ili iweze kufunguliwa mapema. 

Akiwa Ziara Jimboni Kutembelea na kukagua utekelezaji wa Ilani, Dkt Jafo ametembelea mradi wa Ujenzi wa Shule Mpya ya Sekondari Visiga iliyopo kata ya Msanga. Dkt Jafo amesema ameridhishwa na ujenzi wa shule hiyo ya kimkakati inayolenga kuwapunguzia wanafunzi umbali mrefu kwenda Shule ya Sekondari Janguo. 

"Sekondari hii iko kimkakati zaidi, watoto wa bembeza wanakuja hapa, watoto wa Visiga wanakuja hapa na hata watoto wa Marui wanakuja hapa"

"Historia inasema watoto wetu kutoka huku visiga wanahangaika, mtoto atoke visiga mpaka akapande ule mlima aende janguo watoto wanateseka, wengine wanakatisha masomo kwasababu ya umbali. 

Dkt. Jafo ameiagiza Ofisi ya Mkurugenzi kukamilisha ujenzi wa Miundombinu ya Vyoo vya Walimu ili shule hiyo ianze kupokea wanafunzi wakati akitenga Bajeti kutoka Mfuko wa jimbo kujenga Nyumba ya Mwaalimu. 

"hapa nitoe maagizo kwa Mkurugenzi, fanya utaratibu anza kujenga choo cha walimu, na choo hicho kijengwe haraka lengo ni kwamba shule hii ianze kufanya kazi, hizi harakati zingine tunapambana nazo kupata nyumba ya Mwalimu na baadae Jengo la utawala"


Pia Dkt Jafo amemuagiza Afisa Elimu Sekondari kushughulikia kibali kutoka kwa mamlaka husika ili kufanikisha jitahada za kuifanya shule hiyo kufanya kazi. 


"Afisa Elimu Wilaya hakikisha sasa weka utaratibu hata kupata Provisional Permit watoto waanze kusoma hapa miezi michache ijayo. Hii Shule haitakiwi iendelee kubaki hapa, na hii kazi nyingine walimu wanaofisi hizi mbili watajibana, najua changamoto ya Walimu, sasa hivi Serikali inaajiri Walimu naamini tutapata vijana wengine watasaidia hii Shule ifanye vizuri".


Shule ya Sekondari Visiga ina jumla ya madarasa saba ya kisasa yaliyokamilika pamoja na Ofisi mbili za Walimu. 

Aidha Dkt Jafo amesema maboresho makubwa yamefanyika katika Shule za Sekondari Wilayani humo pamoja na kujenga shule mpya za Sekondari Saba ikiwemo na Shule inayobeba jina la Wilaya "KISARAWE SEKONDARI" Iliyopo kata ya Kazimzumbwi, zingine ni Dkt. Jafo Sekondari, Mloganzila Sekondari, Videte Sekondari, Kitanga Sekondari, kisangire Sekondari pamoja na Visiga Sekondari.

Post a Comment

0 Comments