KAZI NA MAJUKUMU YA KWANZA YA RAIS SAMIA
Kwa kuzingatia mazingira ya dharura ambayo MH.Dk SAMIA MSULUHU HASSAN. Akiapishwa kuwa Rais na mkuu wa nchi alikuwa na majuku ya awail ya fuatayyo.
Kuwaondolea hofu wa Tanzania. Hili kimsingi lilikuwa jukumu kubwa la kwanza kama mkuu wa nchi kwa kuwa wananchi walikuwa na mawazo mseto na hili alifanya kwa ufasaha mkubwa kweye somo la urai tunajifunza kuwa kazi ya Rais ni mfariji mkuu wa nchi.
Kuwaunganisha wa Tanzania hapa ndipo tunapoona mantiki ya R4. Hasa ile dhana ya maridhiano. (reconciliation) kwa kuzingatia kuwa nyenzo kuu ya maendeleo ni umoja na mshikamano kama taifa tuwe kitu kimoja kulijenga, Amani ikitawala inahuisha ari ya kazi na uzalishaji wa kiuchumi katika taifa,hivyo dhana ya maridhiano na upatanisho imekuwa nguzo kubwa ya kudumisha upendo na uzalendo wa nchi na pia heshima ya binadamu, ikumbukwe kuwa katika medali za siasa hapo awali kulikuwepo na zuio la vyama vya siasa kufanya mikutano ya hadhara katika kunadi sera na falsafa ya vyama na vyombo vya habari kuhisi kuto tendewa haki ya kuandika habari kwa uhuru kama ilivyo sheria mara tu baada ya kuapishwa aliweza ruhusu shughuLi hizo zote kufanyika kwa mujibu wa katiba na sheria za nchi hii ili ashiria kwamba Rais analenga kuwaunganisha waTanzania wawe kitu kimoja (mshikamano) ili kuleta maeendeleo. pia aliwaachia waliokuwa magerezani wale wenye kesi zenye mnasaba na siasa na pia kuwaita viongozi wa vyama vya siasa kufanya nao mazungumzo ambayo hatimaye hii imepelekea taifa kuwa na utulivu mkubwaa hapa tuna kila sababu ya kumpongeza MH.RAIS SAMIA SULUHU HASSAN.
Kuimarisha diplomasia ya kikanda na dunia kwa ujumla na hususani diplomasia ya kiuchumi kwa mujibu wa sera ya mambo ya nje (Tanzania foreign policy) ya nchi yetu iliyo nzishwa mnamo 2001 ikichukua taswira ya kuimarisha diplomasia ya uchumi hususani kuvutia wawekezaji na technolojia na utalii ikiwemo utalii wa mikutano na matibabu katika hospital ya Taifa Muhimbili na Benjamini mkapa Dodoma.
TUZIFAHAMU 4R ZA RAIS SAMIA NA TIJA YAKE KWA UMOJA WA KITAIFA
1.MARIDHIANO (RECONCILIATION) hii ni kwamba sisi wa Tanzania tuweze kuishi na kudumisha tunu ya Amani,umoja na mshikamano kwa kuzingatia msingi ya maridhiano kwa jambo au mitazamo mseto inapotokea. Na hii si kwa taifa bali hata ngazi ya familia tukijenga desturi ya maridhiano tuta kuwa na umoja na mshikamano na hatimaye upendo miongoni mwetu nahii itapunguza migogoro ya ndoa hata taraka kupungua ,hivyo falsafa ya maridhiano isibaki tu katika medali za siasa na vyama vya siasa bali tuiishi kwa vitendo katika jamii zetu. mfano tumeshuhudia CCM mkoani Mwanza wakichanga fedha kwa ajili ya kumsaidia ndg Tundu Lissu aweze kutengeneza gari yake hii imedhihirisha kuwa kukinzana kimtazamo katika siasa hakuna madhara ya kushindwa kusaidiana katika mambo ya kijamii hili ni jambo la kupongezwaa na limedhihirisha kuwa CCM Kama taasisis ina iishi dhana ya maridhiano Na hii ndio siasa safi aliyo tu husia Baba wa taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwamba ili taifa lolote lipate maendeleo linahitaji siasa safi na uongozi bora hivyo CCM imedhihirisha ina ishi kwenye msingi ya siasa safi.
2.USTAHIMILIVI ( RECILIANT) Huu ni msingi wa demokrasia kuvumiliana pale una pokosolewa na hii inasaidia kujenga taifa la watu wenye umoja na mshikamano. Mfano hai tumeshuhudia kiongozi mkuu wa nchi kubaki katika hali ya utulivu na hatimaye hutoa majawabu yasiyo ksi jazba wala kinyongo kwa wanao mkosoa.hii ina tuu fundisha kuwa ustahimilivu nunguzo muhimu sana katika siasa na jamii kwa ujumla.
Kwa kuwa kiongozi mkuu wa nchi amethibitisha kuwa ustahimilivu ni nyenzo nzuri ya kuongoza na kuishi na jamii nasi pia tuiishi hio zana ya ustahimilivu.
3.MAGEUZI AU MABADILIKO.-(REFORMS). Hii dhana ina tuhimiza tuwe watu wa mabadiliko na tuwe tayari kwamabadiliko. Hata historia ina tuonyesha kuwa mwaka 1991 kwenye tume ya nyarari ili kuja na maoni ya wananchi juu ya mfumo wa chama kimoja maoni ya wananchi 21% walitaka mfumo wa vyama vingi na 79% litaka mfumo wa chama kimoja ueendelee nah ii imethibitisha namna ilivyo kuwa vigumu watu kupokea mageuzi ya mifumo ila kwa namna Mh Rais Samia anavyo zingatia mageuzi ya mifumo tumeona kuundwa kwa tume mfano tume ya haki jinai. Hii yote ni kuhakikisha mageuzi yana kuwa ya kimifumo kwa mstabali wa taifa.
4.KUJENGA UPYA.(RE BULD).Hii falsafa ina tuasa kujenga upya pale ambapo pana changamoto ili tuweze kwenda mbele kama taifa.mfano tumeona mabadiliko ya sharia ya uchaguzi. T toka kuwa tume ya Taifa ya uchaguzina kuwa Tume Huru ya uchaguzi. Hii ni matokeo chanya ya hii falsafa ya kujenga upya.
HITIMISHO
0 Comments