Ticker

6/recent/ticker-posts

RAIS SAMIA AWASILI HARARE NCHINI ZIMBABWE KWA AJILI YA KUSHIRIKI MKUTANO WA 44 WA WAKUU WA SADC

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Robert Gabriel Mugabe kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa 44 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) Harare nchini Zimbabwe tarehe 15 Agosti, 2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akipokea zawadi ya Ua kutoka kwa mmoja wa Watoto waliofika kumpokea katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Robert Gabriel Mugabe, Harare nchini Zimbabwe tarehe 15 Agosti, 2024. Mhe. Rais Dkt. Samia anatarajia kushiriki Mkutano wa 44 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa (SADC) nchini humo tarehe 16-17 Agosti, 2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akimsalimia mmoja wa Watoto mara baada ya kuwasili Harare nchini Zimbabwe tarehe 15 Agosti, 2024.

Post a Comment

0 Comments