NA MWANDISHI WETU
KAMPUNI ya Oryx Gas imeendelea kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa kuendesha mashindano ya kupika kwa gesi ya Oryx kwa Mamalishe 1000 mkoani Mbeya katika kumuunga mkono Rais Samia kudhamiria ifikapo mwaka 2024 asilimia 80 wananchi wawe wanatumia nishati safi.
Akizungumza
na waandishi wa habari mkoani hapa leo Agosti 27,2024 jijini Mbeya ,
Meneja Miradi ya Nishati Safi kutoka Kampuni ya Oryx Gas Tanzania Peter
Ndomba amesema mashindano hayo yanatija kubwa kwa Mama Lishe na Baba
Lishe kwani wanatambua kundi hilo ndilo linaloathirika kiafya kutokana
na kutumia kuni na mkaa kwa muda mwingi.
"Mama Lishe anakaa muda
mrefu katika anapopika kwa kutumia na mkaa kwani tunaambiwa wananchi
wengi wa Tanzania wanafariki kila mwaka kwa kutokana na matatizo ya
kupumua au matatizo ambayo yanatokana na madhara ya kuni na mkaa.
"Sasa
katika hao watu tunaweza kusema Mama Lishe ndio waathirika wakubwa ,
kwa hiyo ni jamii ambayo sasa hivi sisi Oryx tunamkakati wa kuhamasisha
iachane na kuni na mkaa kwasababu wao wanakaa muda mrefu katika kupika
kila siku ndani ya siku 365,"amesema Ndomba.
Amesisitiza kwa hiyo
Mama Lishe na Baba Lishe wakiamua kubadilika na kuanza kupila kwa
nishati safi kutawasaidia kukabiliana na changamoto za kiafya na hivyo
kuokoa maisha yao, hivyo mashindano ya kupika kwa gesi ya Oryx kunalenga
kuliepusha kundi hilo dhidi ya madhara yanayotokana na kuni na mkaa.
"Lengo
la mashindano haya ni katika muendelezo uleule ambao Oryx tumeuanza
muda mrefu wa kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia katika
mapishi yake.
Kwa hiyo ujumbe wetu kwa watu watumie gesi katika
kupika mapishi.Tunaamini nishati safi ya kupikia ni suluhisho la
changamoto nyingi hasa za kiafya,kimazingira na kiuchumi,"amefafanua.
Pia
amesema Oryx wanaamini wanalojukumu la kuendelea kuhamasisha nishati
safi na ndio maana tumeleta mashindano haya katika eneo la wazi ili kila
mtu aone .
Kwa upande wao baadhi ya Mama na Baba Lishe
wanaoshiriki mashindano hayo wamempongeza Mbunge wao Dk Tulia Akson
pamoja na Oryx Gas kwa KUANDAA mashindano hayo ambayo yanakwenda
kuongeza hamasa ya matumizi ya nishati safi katika shughuli zao za
kupika.
Akizungumza kuhusu mashindano hayo
Mama Lishe Yusra
Ismail anayefanya shughuli zake za mama Lishe eneo la Sabasaba jijini
Mbeya amesema mashindano hayo yanamanufaa makubwa kwao kwani wanapata
elimu kuhusu umuhimu wa kutumia nishati safi lakini na matumizi salama
ya nishati hiyo.
"Gesi ya Oryx imekuwa ikitusaidia katika
shughuli zetu za mapishi, tunafanya shughuli zetu kwa haraka,"amesema
huku akieleza kutumia kuni na mkaa kunapoteza muda lakini pia
wanaathirika kiafya.
Ameongeza kuwa wanamuunga mkono Rais
DK.Samia Suluhu Hassan kwa kuhamasisha matumizi ya nishati safi nchini
kwasababu nishati ya gesi ni nzuri na inasaidia katika shughuli zao.
Wakati
huo huo Mama Lishe Sabrina Anold anayetokea Kata Ilomba ameseema
programu ya nishati safi ya kupikia katika Jiji la Mbeya imekuwa na
faida nyingi kwani Mama na Baba Lishe wameendelea kuhamasika kwa kutumia
nishati safi ya kupikia katika shughuli zao.
"Dk.Tulia kwa
kushirikiana na Oryx Gas wametusaidia sana kwani awali tulikuwa
tunatumia kuni na mkaa ambapo tulikuwa tunapoteza muda ,kwahiyo baada
ya kuja nishati safi tunaweza kutumia muda mzuri na kingine imetusaidia
katika eneo la afya kwani wengine macho yamepoteza kuona vizuri
kwasababu ya Moshi kwa kutumia kuni." .
Wakati huo huo Baba Lishe
Yusuph Maumba ambaye ni mshiriki wa shindano la mapishi amesema
mashindano hayo yanaongeza hamasa ya kutumia nishati safi ya kupikia na
hasa gesi ili kuepuka kuharibu mazingira kwasababu ya kupika kwa kuni na
mkaa.
"Kiukweli tutandelea kumuunga mkono Rais Dk. Samia kwa
kutunza mazingira kwa kutumia nishati ya gesi katika kupikia na uzuri
chakula kinachopikwa kwa gesi ni kizuri na kitamu . Nimefurahishwa sana
na mashindano hayo."
Ameongeza kuwa kutumia kuni na mkaa
kunachangamo nyingi kwanza mkaa ni wa msimu kwasababu nyakati za mvua
mkaa unakuwa umeloa na wakati mwingine unauziwa chenga.
Kwa
upande wake Baba Lishe Zakaria Msigwa amesema wanamuunga mkono Rais
Samia kwa kutumia nishati safi ya kupikia sambamba na kuhamasisha
wengine kutumia nishati hiyo kwani dhamira ya Rais ni kuona wananchi
wake wanatumia nishati safi ya kupikia na kuachana na nishati chafu.
Amewashauri
wanaotumia kuni na mkaa kuachana na matumizi ya nishati chafu na kisha
kuanza kutumia nishati safi huku akiwaomba Oryx kuendelea kutoa elimu ya
umuhimu wa kutumia nishati pamoja na kuendelea kugawa mitungi ya gesi
na majiko yake.
0 Comments