Ticker

6/recent/ticker-posts

JUBILEE INSURANCE WAJA NA KAMPENI YA ISHI HURU KWA AJILI YA KUJENGA UELEWA MASUALA YA BIMA

Na Said Mwishehe, Michuzi TV

KAMPUNI ya Afya ya Jubilee Insurance imezindua kampeni yake mpya ya Ishi Huru kwa lengo la kuhakikisha Watanzania wanaondolewa mzigo wa maisha ukiwemo wa matibabu ya afya kwa kutumia bima ambayo kila Mtanzania anaweza kuwa nayo sambamba na kuhamasisha na kujenga uelewa wa umuhimu wa bima ya afya.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Ishi Huru Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bima ya Afya ya Jubilee Dk.Harold Adamson amesema kampeni hiyo mbali ya Tanzania inahusisha nchi za Uganda na Kenya.

"Kampeni yetu ambayo tumeizindua leo rasmi tunaamini itasaidia kuwaweka huru watanzania wenzetu kuishi na kuwatua mizigo ya matibabu ya kiafya kwani kampuni yetu itawapa fursa ya kupata bima zetu za afya na bima ya maisha katika kubaliana na matatizo mbalimbali.

"Mtakubaliana nami masuala ya bima ya afya yamekuwa yakionekana kama yanawahusu matajiri, wenye vipato vya kati au waliojiriwa lakini tunakuja mbele yenu kuwapa fursa kupitia kampeni hii yenye lengo la kuwafikia Watanzania wote wa vipato tofauti ambao wataweza kufikiwa na kampeni hii ili watumie bima zetu."

Amefafanua neno ishi limetafsiriwa kwa maana mbalimbali lakini wao Jubilee imewatafsiri na neno hilo la kuishi huru bila kuwa na mawazo kwa chochote ambacho kinaweza kutokea kama kuugua huku akiongeza kuwa ni imani yao kupitia kampeni hiyo watu wengi watatambua na kupata uelewa nini bima ya fya na bima ya Maisha.

Pia amesema kampuni hiyo imejipanga vema kuendelea kutoa huduma bora kwa wateja wao na ambao sio wateja wao wataendelea kuwaelimisha kupitia kampeni yao ya Ishi huru.

Ametumia nafasi hiyo kutoa mwito kwa watoa huduma za afya kuweka gharama rafiki za matibabu badala yake waweke viwango ambavyo vitakuwa stahimilivu kwa Watanzania wa hali zote.Kwasasa uelewa wa matumizi ya bima nchini ni chini ya asilimia moja, hivyo wadau wanapaswa kujua kuwa wanakazi kubwa ya kufanya ili kuchochea watanzania wa hali zote kujiunga na bima ya afya.

"Kuna haja ya kwa watoa huduma za afya kuweka gharama ambazo ni stahiki, hizi fedha ambazo tunazitoa kwa ajili ya kulipia gharama za matibabu ni watu hivyo zitumike kwa usahihi na iwe inayostahamilika ili kila mtanzania awe na uwezo wa kulipa.Tunafahamu watanzania wangeweza kulipa cash lakini wameona wapiti katika kampuni za bima ili kupata unafuu."

Pamoja na hayo ameipongeza Serikali kwa kuweka mazingira mazuri kwa sekta binafsi na taasisi za bima ya afya kufanya kazi baada ya Rais Samia Suluhu Hassan siku chache zilizopita kusaini muswada wa bima ya afya kwa wote.

"Tunaishukuru Serikali kwa kuweka mazingira mazuri ya sisi tunaojihusisha na masuala ya bima ya afya kufanya kazi katika mazingira mazuri, tumeendelea kuwa wabunifu na sisi Jubilee tuko mikoa yote na kubwa Zaidi tunafanya kazi kidijitali."

Awali Ofisa Mtendaji Mkuu wa Jubilee Life, Helena Mzena ameeleza kwa kina umuhimu wa kampeni hiyo na kusisitiza itajikita kutoa elimu na kuendeleza uelewa kwa wananchi kujua matumizi sahihi ya bima na kuongeza kuna mtazamo kwa watu walio wengi kuwa bima ni ya watu fulani."Kupitia kampeni ya Ishi Huru tunaamini tutajenga uelewa wa wananchi kutambu umuhimu wa bima."

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Afya ya Jubilee Dk.Harold Adamson ( kushoto) na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Jubilee Life Helena Mzena wakizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Ishu Huru

Post a Comment

0 Comments