Ticker

6/recent/ticker-posts

FCS YAINGIA MAKUBALIANO HAYA NA TCRA CCC



Foundation for Civil Society (FCS) na Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano la Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA CCC) wamesaini  makubaliano ya miaka mitatu yenye lengo la kuimarisha juhudi za kulinda haki za Watumiaji wa huduma katika Sekta ya Mawasiliano Tanzania.

Akizungumza na waandishi wa Habari leo Jijini Dar es Salaam katika hafla ya kusaini makubaliano hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa FCS Justice Rutenge amesema ushirikiano huo unatambua umuhimu wa kuwalinda Watumiaji dhidi ya mbinu za kibiashara zisizo za haki katika soko.

Ameongeza kuwa ubia huo una lengo la kuhakikisha kuwa haki na uwajibikaji katika kutoa huduma kwa Watumiaji na kuwawezesha kufanya maamuzi sahihi wanaponunua na kutumia bidhaa za huduma.

“Kulinda haki za Watumiaji (consumer protection) kunachangia Maendeleo ya masoko na ukuaji wa Biashara hivyo makubaliano haya yatarahisisha utekelezaji mzuri wa haki za watumiaji wa Mawasiliano” Amesema Rutenge.

Amesema Biashara zinazoheshimu sera za kulinda Watumiaji na kuwapa wateja wao kipaumbele hujijengea hadhi na kuziweka katika nafasi nzuri kiushindani na kuzihakikishia Biashara hizo uwepo wa wateja wa uhakika na kuweka msingi mzuri wa ukuaji.

Hata hivyo amesisitiza kuwa umuhimu wa asasi za kiraia kushiriki katika kuimarisha mifumo ya kulinda na kutetea haki za Watumiaji wa huduma na bidhaa za Mawasiliano.

Ameongeza kuwa kupitia mradi huo watajenga uwezo wa asasi za kiraia kuboresha uwiano katika Sera na hatua zinazochukuliwa katika ngazi ya chini, hasa pale ambapo wadau na Watumiaji wa bidhaa Wana uelewa mdogo kuhusu haki na majukumu yao ili kukuza uelewa wa Watumiaji wa huduma na bidhaa.

Amesema watumiaji wana haki ya kupata Suluhu ya haki kwa madai ya msingi, Elimu na uwezo kuhusu bidhaa, huduma na Haki zao na uhakika wa ubora wa bidhaa na huduma.

Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa TCRA CCC Mary Msuya amesema Baraza limeanzihwa kwa lengo la kuwakilisha maslahi ya Watumiaji wa huduma za Mawasiliano za TEHAMA, huduma za Utangazaji, huduma za posta, na vifurushi na Vipeto.

Ameongeza kuwa Baraza linatekeleza majukumu yake ya kuwakilisha Watumiaji wa huduma na bidhaa za Mawasiliano kwa kushauriana na wadau ambao ni Serikali, TCRA, watoa huduma na Watumiaji wenyewe.

Hata hivyo amesema watumiaji wa huduma ya Mawasiliano wanawajibu wa kuzingatia sheria na wao kama Baraza wanahakikisha kuwa haki zao zinalindwa.

Post a Comment

0 Comments