Na Mwandishi Wetu
Tume ya Mipango na Timu kuu ya Kitaalamu ya Uandishi wa Dira 2050 wamekutana katika Mkutano Maalum uliohudhuuriwa na wajumbe wake kujadili Mustakabali na mwenendo wa ukusanyaji wa maoni ya Wananchi kuhusu Dira ya 2050.
Tume hiyo ya Mipango imewahakikishia wananchi usiri katika maoni watakayoyatoa kwa ajili ya kutengeneza Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.
Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Lawrence Mafuru, alisema hayo jana wakati wa kikao cha Kamati ya Usimamizi wa Dira, kwenye kikao hicho cha Wajumbe wa Tume ya Mipango, Timu ya kitaalamu na uandishi wa dira ya Maendelo 2050.
Aidha, amewataka wananchi kuendelea kujitokeza kwa wingi kutoa maoni yao katika mfumo tofauti uliowekwa, ili kuhakikisha kila mmoja anashiriki kutengeneza nyaraka hiyo muhimu kwa maendeleo ya Taifa letu.
Wajumbe hao walikutana kwa ajili ya kupata picha kamili ya walipotoka na wanapokwenda katika kutengeneza dira hiyo, katika Mkutano huo uliongozwa na Prof Kitilya Mkumbo na kuhudhuriwa na wajumbe wake akiwemo Waziri wa Fedha, Dk. Mwigulu Nchemba aliyehudhuria Mkutano huo kwa nafasi yake kama Mjumbe.
"Tumekutana ili kujadili kwa kina na kujiwekea mkakati na malengo ambayo si yakufikirika, lakini kutekelezeka,” alisema.Mafuru kikao hicho kiliangakia Mapitio ya utekelezaji wa Dira 2025 Muhtasari wa utekelezaji wa Dira 2050 pamoja na Utafiti wa kaya na maoni yaliyojazwa kwa kutumia simu/mtandao (USSD/ Web portal) .
Mafuru alisema wananchi wanaendelea kujitokeza kwa wingi kutoa maoni yao kwa kuzingatia vipengele vya dodoso, huku wakitakiwa kuongeza maelezo na taarifa za ziada ambazo ni muhimu kuzingatiwa katika Dira hiyo.
“Taarifa watakazotoa wananchi zitatumika katika maandalizi ya Dira na hivyo nawahakikishia usiri wa taarifa zao. Serikali inatambua kuwa, maono na maratajio ya Watanzania na mbinu za kuyafikia zinatokana na Watanzania wenyewe kupitia ushirikishwaji madhubuti katika maandalizi na utekelezaji wa mipango ya maendeleo,” alisema.
Kwa mujibu wa Mafuru, ili kuhakikisha Dira hiyo inabeba maono na matarajio ya Watanzania kwa miaka 25 ijayo, ni muhimu wananchi na wadau wote wa maendeleo kushirikishwa kikamilifu katika mchakato wa maandalizi ya Dira tangu hatua za awali hadi kukamilika kwake.
“Lengo la kikao hiki ni kungalia sasa mambo muhimu ambayo matarajio yetu kama Nchi yaliweka na kuangalia kama yalifikiwa na kuangalia kule tunakokwenda na yale tunayoyachukua naa kuendelea nayo mbele,” alisema.
Alisema kinachotakiwa ni kuangalia maoni na kuwa na sura halisi ya uchumi sanjari na malengo yanayotarajiwa kuyaona.
0 Comments