Ticker

6/recent/ticker-posts

Waziri Aweso aonya udokozi wa Fedha za mradi wa Hatifungani

WAZIRI wa Maji Jumaa Aweso akizungumza wakati halfa ya utiaji saini ya ya mikataba utekelezaji wa miradi ya maji kwa fedha za hati fungani kati ya Tanga Uwasa na Wakandarasi STC Contracstion Limited na China Railway 7 Group Limited katika halfa iliyofanyika kwenye ofisi za Mamlaka hiyo.

Na Oscar Assenga, TANGA

WAZIRI wa Maji Jumaa Aweso amesema hatarajii kuona fedha zilizochangwa na wananchi kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya hati fungani zinadokolewa au kuchezewa badala yake wahakikishe zinatumika kwenye malengo yaliyokusudiwa na kurejeshwa kwa utaratibu waliojiwekea.

Aweso aliyasema hayo mwishoni mwa wiki wakati wa halfa ya utiaji saini ya mikataba utekelezaji wa miradi ya maji kwa fedha za hati fungani kati ya Tanga Uwasa na Wakandarasi STC Contracstion Limited na China Railway 7 Group Limited katika halfa iliyofanyika kwenye ofisi za Mamlaka hiyo

Alisema kwamb wanapaswa kuhakikisha wanazilipa ili wapate nguvu na maeneo mengine waweze kufaidika na huo ndio uelekeo wa Serikali kwa mamlaka za maji nchini.

Alisema kwamba jambo ambalo limefanywa na mamlaka hiyo ni kubwa huku akimuangiza Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Agnes Meena kumfikisha salamu katibu Mkuu lazima utendaji wake na usimamizi katika mradi huo pamoja na ufuatiliaji uwe wa kipekee ili kufanikisha dira na dhamira ya Rais Dkt Samia Suluhu.

“Tunapozungumza fedha za wananchi wameweza katika hati fungani na mwananchi namba moja aliyetoa fedha kwa ajili ya kusapoti maji katika Jiji la Tanga ni Rais Dkt Samia Suluhu hivyo niwasihi tusidokee na tusichezee huu mradi tuende kutumiza malengo ya Rais “Alisema Waziri Aweso

Hata hivyo aliwataka wakandarasi ambao wamepata dhamana ya kutekeleza mradi huo wao kama Wizara jicho lao litakuweo hapo muda wote kusimamia na kufuatilia hivyo wanahitaji kuona tija kubwa katika utekelezaji wa miradi hiyo.

“Bodi ya Tanga Uwasa tunapozungumzia hati fungani ni fedha za wananchi wamesema hivyo fedha kama wamekopeshwa lazima kuzirejesha na faida wasije wakawa watu wa maneno hawataeleka ile nia njema nzuri ambayo waliopanga kuifanya itabadilisha taswira ya Taasisi yenu…niwapongeze Tanga Uwasa ukiwa baba au mzazi ukiona mtoto wako anafanya kazi nzuri jukumu lao ni kumuombe dua hivyo mimi ninawaombe dua”Alisema.

Awali akizungumza wakati wa halfa hiyo Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Tanga Uwasa Dkt Ally Fungo alisema kwamba wameingia kwenye historia katika miradi waliosaini hapo wanakwenda kuitekekeza ni sehemu ya mradi mkubwa wa hati fungani kama alivyoeleza Waziri kinachotokea ni wananchi kuwekeza kwenye huduma ya maji.

Alisema fedha zao zinaende kutoa huduma ya maji na hivyo baadae kupata faida jambo hilo ni la kwanza kufanyika hapa nchini kupitia mamlaka hiyo huku akimshukuru Rais Dkt Samia Suluhu wazo hilo lilipofika kwake aliona ni njia nzuri ya kusaidia serikali kugharamia miradi ambayo serikali inapata ugumu kuigharami kwa sababu ya uwepo wa miradi mingine mikubwa ya kipaumbele .

“Hivyo akikubaliana na wazo hilo litekelezwe na amekuwa pamoja nasi muda wote mpaka sasa na Rais amewekeza ni moja ya watu waliowekeza kwenye hati fungani na wengine ambao wamewekeza ambao wamejitokeza na kukudhi kwa muda mfupi kupata kiasi cha zaidi ya Sh.Bilioni 53 walichokuwa wakikihitaji lakini kimevuka lengo mpaka Bilioni 54 “Alisema Mkurugenzi huyo wa Bodi ya Wakurugenzi.

“Niwashukuru wawekezaji ambao wamewekeza kwenye hati fungani niwaambie fedha zenu sipo salama na hazitapotea na hakuna hata moja na zitafanya kazi iliyokusudiwa na tumejipanga kufanya mradi huo na Mhe Waziri usiwe na wasiwasi ikifika wakati wa kulipana faida na tutaanza na mwezi Octoba mwaka huu na Aprili mwakani kila mwaka na wamejipanga kutekeleza hilo” Alisema

Naye kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Agnes Meena akizunguma katika halfa hiyo alimshukuru Rais Dkt Samia Suluhu kwa kuendelela kuipa kipaumbele cha hali ya juu sekta ya maji na hivyo kuwawezesha kuendelea kutekeleza majukumu yao kwa wepesi.

Naye kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga Gilbert alisema kwamba mkoa huo umeendelea kuimarisha hali ya upatikanaji wa huduma ya maji safi na usafi wa mazingira kwa wananchi ambapo miradi mbalimbali ya kimkakati inaendelea kukamilika na kuwezesha upatikanaji wa huduma bora

“Tunaishukuru Serikali kwa kuendelea kuipa nguvu sekta ya Maji kwa mkoa wa Tanga jumla ya miradi 67 yenye thamani ya Bilioni 89.67 inatekelezwa kupitia Ruwasa na miradi 13 yenye thamani ya Bilioni 11.32 inatekelezwa na Tanga Uwasa hivyo tunaendelea kuishukuru serikali kwa kuendelea kupambania wananchi wa mkoa huu na kuendelea kuimarisha shughuli za kijamii na kichumi”Alisema

Post a Comment

0 Comments