Rais wa Jamhuri ya Msumbiji Mheshimiwa Felipe Nyusi amekutana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi Ikulu Zanzibar.
Akizungumza na Dkt. Mwinyi Mheshimiwa Nyusi alitumia nafasi hiyo kumuaga kwa kuwa amemaliza kipindi chake cha uongozi nchini Msumbiji na kumshukuru kwa Ushirikiano aliompatia alipokuwa Waziri wa Ulinzi wa Tanzania.
Amemuahidi kuwa Msumbiji itaendelea kudumisha uhusiano na ushirikiano wake na Tanzania haşa ikizingatiwa historia ya uhusiano uliopo kati ya Tanzania na Msumbiji
Naye Mhe. Dkt. Mwinyi amemshukuru Mhe. Nyusi kwa kumtembelea Zanzibar na kumkaribisha kutembelea Zanzibar wakati mwingine.
0 Comments