Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, ametembelea Jengo la LATRA lililopo kwenye Maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara Saba Saba na kushuhudia shughuli za Udhibiti Usafiri Ardhini zinavyofanywa na LATRA.
Akitoa maelezo katika jengo la LATRA, Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano LATRA, Bw. Salum Pazzy, amesema kuwa LATRA inaongeza ufanisi katika huduma zinazodhibitiwa kwa kutumia mifumo ya TEHAMA, ikiwa ni pamoja na Mfumo wa Kufuatilia Mwenendo wa Mabasi na Mfumo wa Taarifa kwa Abiria unaomuwezesha abiria kujua basi lilipo, muda wa kuwasili kituoni na kukagua mwendo kasi wa basi alilopanda
Maonesho haya yanafikia kilele leo Julai 13, 2024 na kufungwa rasmi na Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi katika Viwanja vya Julius Nyerere, Dar es Salaam.
0 Comments