Ticker

6/recent/ticker-posts

NIDA YAWATAKA WANANCHI WALIOJIANDIKISHA WAKACHUKUE VITAMBULISHO

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

MAMLAKA ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) imewataka wananchi waliojiandikisha katika ofisi za mitaa, vijiji pamoja na shehia kwa upande wa Zanzibar kujitokeza kuchukua vitambulisho vyao ambavyo tayari vinapatikana katika maeneo yao.

Akizungumza katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam, Sabasaba, Mkuu wa Kitengo Cha Mawasiliano NIDA, Geoffrey Tengeneza amewasihi wananchi kuona umuhimu wa kufuata vitambulisho vyao na kuachana na mazoea ya kuona kwamba namba pekee ya NIDA ndio inawatosheleza katika kupata huduma.

"Ni waombe wajitokeze kuchukua Vitambulisho vyao,hii kudhani siku zote utatumia namba za kitambulisho cha utaifa,tukiamua kusitisha namba ya utambulisho wa Taifa,Utapata shida" amesema Tengeneza.

Aidha amesema ambaye yuko mbali na alipojiandikisha anapaswa kuwatumia watu wa karibu kwa kuandika barua akimtambulisha ndugu atakayemchukulia kitambulisho akiambatanisha saini na muhuri wa Serikali ya Mtaa.

Amesema vitambulisho vya watu waliofariki, serikali za vijiji wamepatiwa utaratibu kwa ajili ya kuvirejesha katika ofisi za NIDA.

Pamoja na hayo amesema katika Maonesho hayo Sabasaba wamekuwa wakitoa huduma namna ya kujaza fomu kwa usahihi, kutoa fomu kwa ajili ya kujindikisha, kutoa namba kwa waliojiandikisha na kukitazama kitambulisho ambacho tayari kimetoka na sehemu kilipo.

Tengeneza amesema huduma nyingine ambayo wamekuwa wakiitoa katika Maonesho hayo ni kushughulikia vitambulisho ambavyo tayari vimetoka lakini vinachangamoto kwaajili ya kuvifanyia marekebisho.

Post a Comment

0 Comments