Katibu wa Mbunge Godfrey Nchimila akiendelea kukabidhi jezi na mpira kwa kila timu zinazoshiriki ligi ya Butondo Kishapu/Shagy Cup kwa niaba ya mdhamini mkuu wa ligi hiyo na Mbunge wa jimbo la Kishapu Mkoani Shinyanga Mhe.Boniphace Butondo leo Julai 15,2024 katika uwanja wa mpira Masanga
Mwakilishi kutoka timu ya Ndoleleji Fc Athumani Juma Mwamashimba akipokea jezi na mpira wa timu hiyo Leo kutoka kwa Katibu wa Mbunge Godfrey Nchimila kwa niaba ya Mbunge wa jimbo la Kishapu Mkoani Shinyanga Mhe. Boniphace Butondo leo Julai 15,2024 katika uwanja wa mpira Masanga kwenye uzinduzi wa ligi ya Butondo Kishapu/Shagy Cup iliyodhaminiwa na Mbunge wa jimbo hilo na kuzinduliwa leo.
Mipira na jezi za timu kumi na sita (16) zilizotolewa na Mbunge wa jimbo la Kishapu Mkoani Shinyanga Mhe. Boniphace Butondo kwenye ligi ya Butondo Kishapu/Shagy Cup iliyozinduliwa leo Julai 15,2024 na Katibu wa Mbunge Godfrey Nchimila kwa niaba ya Mbunge wa jimbo hilo Mhe. Boniphace Butondo kwenye uwanja wa mpira wa Masanga.
Picha ya pamoja ya katibu wa Mbunge Godfrey Nchimila na timu ya Mabambasi Fc baada ya uzinduzi leo Julai 15,2024 kwenye uzinduzi wa ligi ya Butondo Kishapu/Shagy Cup Kata ya Masanga Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga waliochapwa bao 1-0 dhidi ya Masanga Fc
Baada ya kabumbu ya msimu wa kwanza kumalizika mapema mwezi huu wa Saba (7) ligi ya Butondo Kishapu/Shagy Cup katika viwanja vya shule ya Msingi Lubaga ligi hiyo imehamia Kata ya Masanga Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga na timu kumi na sita (16) kushiriki.
Ligi hiyo imezinduliwa leo Julai 15,2025 na Katibu wa Mbunge wa jimbo la Kishapu Mkoani Shinyanga Godfrey Nchimila kwa niaba wa Mbunge wa jimbo hilo Mhe.Boniphace Butondo katika uwanja vya mpira Masanga huku akisisitiza kwa timu zote shiriki kucheza kwa upendo na amani kwani michezo ni ajira na afya.
"Ndugu zangu Mbunge wetu Mhe.Butondo amejitolea kudhamini ligi hii kwa kuwapa kila timu mpira na jezi, mbali na hayo bado kuna mambo mazuri ambayo ataendelea kufanya kwenu hiyo yote ni kuhakikisha anatuleta vijana pamoja,jamii ya wana Kishapu pamoja na pia kuibua vipaji vya wachezaji na siku moja kila mwenye ndoto za kuwa mchezaji afikie ndoto hizo hivyo niwatakie kila la heri katika mashindano haya na Mungu awabariki Mcheze kwa amani", amesema Nchimila.
Baada ya uzinduzi wa ligi hiyo kulifuatiwa na mchezo kutoka kwa Mabambasi Fc iliyofungwa bao 1-0 dhidi ya Masanga Fc goli lililofungwa na kiungo Dida Jumanne katika kipindi cha pili cha mchezo huo na kesho Julai 16,2024 watachuana Ndoleleji Fc na Isemelo Fc.
Miongoni mwa timu kumi na sita (16) zinazo shiriki ligi ya Butondo Kishapu/Shagy Cup ni pamoja na
Masanga Fc, Mabambasi Fc, Isemelo Fc, Lagana Fc, Mihama Fc, Mwamadulu Fc, Mwamalasa Fc, Ng"wang'alanga Fc, Mwamashimba Fc, Wabishi Mhunze Fc, Idisa Fc, MwalataFc, Ndoleleji Fc, Pemba Mangu Fc, Mwampo Fc,Stend Masanga Fc.
0 Comments