Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania(TET) Dkt. Aneth Komba ametoa rai kwa wadau mbalimbali wa elimu nchini kutembelea katika katika maonesho ya kibiashara ya kimataifa ya Dar es salaam hususani katika banda la TET ili kuweza kufahamu utekelezaji wa Mtaala ulioboreshwa.
Ameyasema hayo leo Julai 9, 2024 wakati aliopotembelea katika maonesho hayo katika viwanja vya sabasaba jijini Dar ea salaam ambapo ameeleza kuwa TET imeendelea kutoa elimu kwa wadau nchini kwa kuwaelewesha maboresho ya Mitaala yaliyofanyika, ambayo utekelezaji wake ulianza mwezi Januari 2024.
"Wadau tembeleeni katika banda letu hapa mtapata kufahamu masuala mengi kuhusiana na utekelezaji wa Mitaala iliyoboreshwa." amesema Dkt.Komba.
Pia, amesema kuwa TET inaendelea na uuzaji wa vitabu vya kiada kwenye maonesho hayo, hivyo kuwakaribisha wananchi wanaohitaji vitabu vya kiada vya Mitaala yote.
Katika ziara hiyo, Dkt.Komba alipata pia nafasi ya kutembelea katika mabanda mengine yakiwemo NECTA, NACTVET NA TBC.
0 Comments