Mbunge wa jimbo la Kishapu Mkoani Shinyanga Mhe.Boniphace Butondo leo Julai 11,2024 katika viwanja vya hospitali ya Dr. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumzia adhima ya serikali ya awamu ya sita katika kuhakikisha inakabiliana na kuondoa changamoto mbalimbali za wamama wajawazito na wagonjwa wengine baada ya kupokea vifaa tiba vyenye thamani ya Tsh. Mil. 14 kutoka bohari ya dawa MSD kupitia mfuko wa fedha za dunia GLOBAL FUNDS kwa ajili ya vituo vya kutolea huduma za afya Wilayani humo.
Na Sumai Salum - Kishapu
Hospitali ya Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga imepokea vifaa Tiba vyenye thamani ya Tsh. Milioni 10 kutoka bohari ya dawa MSD kupitia mfuko wa fedha za dunia (GLOBAL FUND) kwa ajili ya vituo vya kutoka huduma za afya.
Akisoma taarifa ya upokeaji vifaa tiba hivyo kabla hajavikabidhi kwa Mbunge wa Jimbo la Kishapu Mhe. Boniphace Butondo Leo Julai 11,2024 Afisa afya na Kaimu Mganga mkuu Hospitali ya Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete Wilayani Kishapu Godfrey Kisusi amesema kuwa vifaa hivyo vitaenda kuboresha huduma zaidi kwa wamama wajawazito pamoja na wagonjwa wengine.
Aidha Kisusi ametoa wito kwa wananchi wa Kishapu na maeneo jirani wanatakiwa kuendelea kufika katika vituo vya afya,zahanati na hospitali ya Wilaya pindi wahitajipo huduma za afya kwani huduma sasa ni salama na zenye uhakika.
"Kwanza nipende kutoa pongezi kwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na Mbunge wetu wa Jimbo la Kishapu Mhe. Boniphace Butondo kwa kutupigania wana Kishapu kwa ajili ya uboreshaji katika sekta ya afya", ameongeza Kisusi.
Mbunge wa Jimbo la Kishapu Mhe.Boniphace Butondo akizungumza baada ya kupokea taarifa hiyo amesema serikali ya awamu ya sita imekusudia kuboresha huduma za mama wajawazito ili kuondoa vifo vitokanavyo na uzazi wakati wa kujifungua ndio maana vifaa tiba vingi vinawalenga wao na hata wagonjwa wengine.
"Ndugu zangu baadhi ya wananchi mlioko hapa na viongozi mbalimbali nikiwa mwakilishi wenu nimezungumzia sana mapungufu tuliyonayo Kishapu idara ya afya namshukuru Rais wetu ni msikivu na hata Waziri wa afya Mhe. Ummy Mwalimu kwani miezi michache nyuma alikuja na akajionea mapungufu tuliyonayo na ndio maana Leo hii tunapokea hivi vifaa ambavyo vitasaidia sana kusogeza huduma", amesema Mhe. Butondo
Aidha amewahakikishia wananchi kuwa vifaa hivyo havitabakia katika hospitali hiyo ya Wilaya bali baadhi vitapelekwa kwenye vituo vya afya na zahanati zenye changamoto ikiwemo Kishapu, Negezi, Mondo, Bunambiyu, Songwa na Mwigumbi ili kuwasaidia wananchi na kupunguza changamoto zinazowakabili.
Aidha Kabangala Lubaligi mkazi wa kijiji cha Nobola Kata ya Talaga ameipongeza serikali na Mbunge kwa jitihada wanazoendelea kuzifanya katika kuhakikisha wanakabiliana na kutokomeza changamoto mbalimbali katika sekta ya afya.
Naye Pelazia Christopher mkazi wa Kijiji cha Kijongo ameishukuru serikali na viongozi kwa kuendelea kuhakikisha usalama wa wamama wajawazito kwa kutoa vifaa tiba vingi kwani wamekuwa wahanga wakubwa wa kupoteza maisha wakati wa kujifungua kutokana na upungufu wa vifaa tiba vya kuwasaidia huku akiishauri serkali kuongeza idadi ya watumishi hasa katika vituo vya afya na zahanati.
Vifaa tiba hivyo vilivyotolewa ni pamoja na Bed Labour and delivery 20pcs,Delivery Kit 10pcs,Table examination with pad 10 Pcs,Hospital bed 15pcs,Over bed table Pcs8,Bed side locker metal 15pcs,Drip stand 15pcs,Matresses foam 15pcs pamoja na Bed sheets 120.
Mbunge wa jimbo la Kishapu Mkoani Shinyanga Mhe.Boniphace Butondo leo Julai 11,2024 katika viwanja vya hospitali ya Dr. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumzia adhima ya serikali ya awamu ya sita katika kuhakikisha inakabiliana na kuondoa changamoto mbalimbali za wamama wajawazito na wagonjwa wengine baada ya kupokea vifaa tiba vyenye thamani ya Tsh. Mil. 14 kutoka bohari ya dawa MSD kupitia mfuko wa fedha za dunia GLOBAL FUNDS kwa ajili ya vituo vya kutolea huduma za afya Wilayani humo.
Mbunge wa jimbo la Kishapu Mkoani Shinyanga Mhe.Boniphace Butondo
Afsa afya Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga ambaye ni Kaimu Mganga Mkuu Hospitali ta Dr.J akaya Mrisho Mrisho Kikwete akimwelezea Mbunge wa Jimbo hilo Boniphace Butondo vifaa tiba walivyovipokea kutoka bohari ya dawa MSD kupigia mfuko wa fedha za dunia GLOBAL FUND Leo Julai 11,2024 kabla hajamkabidhi taarifa hiyo
Baadhi ya vifaa tiba vilivyotolewa
Bi. Pelezia Christopher mkazi wa kijiji cha Kijongo Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga akizungumzia namna alivyofurahishwa na serikali ya awamu ya sita ya Dkt. Samia Suluhu kwa kushirikiana na Mbunge wa jimbo hilo Mhe. Boniphace Butondo kupunguza vifo vya mama wajawazito na watoto wachanga Leo Julai 11,2024 wakati wa uwasilishwaji taarifa ya kupokea vifaa tiba hivyo kutoka kwenye uongozi wa Hospitali kwenda kwa Mbunge.
Bw. Kabangala Lubaligi mkazi wa Kijiji cha Nobola Kata at Talaga Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga akizungumza Leo Julai 11,2024 baada ya Mbunge wa Jimbo hilo kupokea taarifa ya upokeaji vifaa tiba kutoka MSD kupitia mfuko wa fedha za dunia GLOBAL FUNDS vyenye thamani ya Tsh Milioni 14 hospitali ya Dr.Jakaya Mrisho Kikwete kwa ajili ya vituo vya kutolea huduma za afya
0 Comments