Ticker

6/recent/ticker-posts

MBUNGE BUTONDO AKABIDHI VIFAA VYA UJENZI VYA SH. MILIONI 86 JIMBONI KISHAPU

 

Mbunge wa Jimbo la Kishapu Mkoani Shinyanga Mhe. Boniphace Butondo ( wa pili kutoka kushoto) akiwakabidhi baadhi ya Madiwani wa Kata zilizopokea vifaa vya ujenzi ikiwemo Saruji kwa fedha za mfuko wa jimbo mwaka 2023/2024 Leo Julai,11,2024

Na Sumai Salum - Kishapu 

Mbunge wa Jimbo la Kishapu Mkoani Shinyanga kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mhe. Boniphace Butondo amekabidhi vifaa vya ujenzi mifuko ya Saruji 1012 na mabati 456 vyenye thamani ya Tsh. 86,000,000 kwenye jumla ya Kata kuni na saba (17) fedha za mfuko wa jimbo  2023/2024.

Akikabidhi Leo Julai 11,2024 alipokuwa Hispitali ya Dr.Jakaya Mrisho Kikwete Wilayani Kishapu Mhe.Butondo amesema ni utaratibu wa serikali kutoa fedha kwenye mfuko wa kila  jimbo kutokana na ukubwa wa eneo na idadi ya watu hivyo walipokea kiasi cha Shilingi 86,000,000 na baada ya Ziara nilizofanya katika jimbo lake alitoa vifaa kulingana na changamoto husika na kata zilizobakia ndizo zinakabidhiwa.

"Nipende kutoa rai kwa wote mtakaochakachua na mtakaochukua vifaa hivi vikafanye kazi sawasawa na mlivyoomba,sina mashaka wa watakaochukua mabati ila wale wa mifuko ya saruji mfanyie kazi kwa haraka mkizingatia muda na ubora wa miradi yenu msifanye uchakachuaji wa namna yoyote ile ukibainika sitokuchekea kabisa",ameongeza Butondo.

Wakitoa shukrani baada ya kupokea mifuko ya saruji na mabati kwa niaba ya Madiwani na Wananchi Diwani wa Kata ya Masanga Mhe. Enock Reuben na Diwani wa Kata ya Kiloleli Mhe. Manyama Nkuba wamemshukuru Mbunge huyo kwa kuahidi kusimamia matumizi ya vifaa hivyo na  miradi iliyokusudiwa kukamilishwa kwa wakati ili wananchi waendelee kupata huduma bora.

Aidha vifaa hivyo vimekabidhiwa kwenye Kata kumi Saba (17 )na  jumla ya Vijiji 27 ikiwa ni pamoja na Mwataga, Ndololeji, Shagihilu, Idukilo, Mwakipoya, Talaga,Ngofila, Itilima, Mwamalasa, Bubiki, Kiloleli, Mwasubi, Sekebugolo, Masanga, Kishapu, Mondo pamoja na Kata ya Igaga kwenye miradi mbalimbali ikiwemo elimu msingi, afya  na maji.
Mbunge wa Jimbo la Kishapu Mkoani Shinyanga Mhe. Boniphace Butondo akisisitiza suala la uaminifu, matumizi sahihi na bora ya vifaa vya ujenzi alivyovigawa Leo Julai 11,2024 ikiwa ni pamoja na  mifuko 1012 ya saruji na mabati 456 kwa Kata 17 (vijiji 27) vya Wilaya hiyo 
Mbunge wa Jimbo la Kishapu Mkoani Shinyanga Mhe. Boniphace Butondo (kushoto) akisaidiana na Diwani wa Masanga Mhe. Enock Reuben(shati jeupe kulia) na pembeni yake ni Diwani wa Kata ya Kiloleli Mhe. Manyama Nkuba kutoa bati kwa ajili ya kupelekwa kwenye kata husika zilizonunuliwa kwa fedha za mfuko wa jimbo 2023/2024 Leo Julai 11,2024

Baadhi ya mifuko ya saruji iliyonunuliwa kwa fedha ya mfuko wa Jimbo la Kishapu Mkoani Shinyanga 2023/2024 iliyokabidhiwa Leo Julai 11,2024 na Mbunge  wa jimbo hilo Mhe. Boniphace Butondo katika hospitali ya Dr. Jakaya Mrisho Kikwete

Gari la mizigo likiwa limebeba mifuko ya Saruji 110 kuelekea Kata ya Ngofila kwa Diwani Mhe. Nestory Ngude baada ya kukabidhiwa hii Leo Julai, 11,2024 na Mbunge wa Jimbo la Kishapu Mkoani Shinyanga Mhe. Boniphace Butondo fedha za mfuko wa jimbo.
Baadhi ya viongozi na wananchi wakiwa kwenye tukio la kukabidhiwa vifaa vya ujenzi mabati na saruji Leo Julai,11,2024 kutokana na  za mfuko wa jimbo na Mbunge wa Jimbo hilo Mhe.Boniphace Butondo
Diwani wa Kata ya Ngofila Mhe.Nestory Ngude(kushoto) na kulia ni Diwani wa Kata ya Ndololeji Mhe. Mohamed Amani wakisikiliza maelekezo ya Mbunge Butondo ya nidhamu matumizi  ya vifaa vya ujenzi vilivyonunuliwa na mfuko wa jimbo hilo la Kishapu Mkoani Shinyanga leo Julai 11,2024
Diwani wa Kata ya Kiloleli Wilayani Kishapu  Mkoani Shinyanga Mhe. Edward Manyama Nkuba akizungumza kwenye zoezi la upokeaji mifuko ya saruji na mabati kutoka kwa Mbunge wa Jimbo  hilo Mhe. Boniphace Butondo Leo Julai 11,2024
Mbunge wa Jimbo la Kishapu Mkoani Shinyanga Mhe. Boniphace Butondo akihakiki taarifa iliyosomwa na Afisa mipango Noela Levira ya ugawaji vifaa vya ujenzi kwa kila Kata husika Leo Julai 11,2024 kabla hajaanza zoezi la ugawaji vifaa hivyo

Post a Comment

0 Comments