Ticker

6/recent/ticker-posts

KSIJ WAIKUMBUSHA JAMII KUPAMBANA NA VITENDO VYA UKATILI, USHOGA.


Na Hamida Kamchalla, TANGA.

WAUMINI wa Dini ya kiislamu, Dhehebu la Koja Shia Ithna Asheri Jamaat (KSIJ) TANGA, wamekusanyika na kuungana kwenye maadhimisho ya kumbukizi ya siku ya Ashuraa, jijini humo.

Ni siku ambayo Mtume, Hussein ibn Ally aliuwawa kikatili katika mji wa Iraq, Karbala akitetea haki za binadamu ambapo hutumia siku hiyo kukabiliana na vitendo vya ukatili wa kijinsia katika Mkoa wa Tanga.

Akiongea wakati wa maadhimisho hayo, Sheikh Shafi Nina amesema waislamu wanaona umuhimu wa kumbukumbu ya mjukuu wa mtume kama kielelezo muhimu kwenye maisha yao ya sasa.

"Siku kama hii tunaiadhimisha Kwa sababu ni msiba mkubwa na ni jambo kubwa ambalo liliugusa uislamu na bahati mbaya liliugusa uongozi wa uislamu kwakuwa alikuwa Kiongozi na mtu mkubwa zaidi Duniani kipindi hicho"

"Kumbukumbu ya kuuwawa Al Imamu Husseni ina mambo mengi, kwanza namna aliyouwawa, wale waliomuua, na mazingira aliyouwawa, yanatufundisha mengi hasa katika uislamu na ubinadamu kwa ujumla" amesema.

Pamoja na mambo meingine waislamu wanatumia siku hii kuitaka jamii na dini zote kuungana na kupambana na vitendo vya ukatili wa kijinsia, imiwemo kupinga ndoa za jinsia moja.

"Kuhusu haya mambo ya ushoga, hiki kipindi tunachoishi sasa ndiyo hasa cha kuitumia dini zaidi kupambana na jambo hili kwakuwa hakuna suluhisho isipokuwa ni dini" amebainisha.

"Na dini zote za mbinguni zinapambana na jambo hili, na hata tukiishi katika jamii zetu za Kiafrika hali hii ni ngumu sana, dini zote ziamke kupambana ndiyo tuweze kuokoka kwa sababu tukiziangalia jamii zetu zinapotea".

Kwa upande wake Mwenyekiti KSIJ Tanga, Samir Bandal amesema tukio la kuuwawa Imamu Hussein limewafundisha mambo ambayo yapo kwenye maisha ya kila siku ya binadamu na kwamba uislamu ni amani na sio vita.

"Hii siku ya Ashuraa inatukumbusha kulinda Uislamu, kuishi kwa uhuru na amani lakini pia Imamu Hussein alikwenda Kalbara siyo kwa nia ya vita bali alifuata amani, amesema Bandal.

"Pia siku hii inatukumbusha kwamba Imamu wetu ametangaza amani pamoja na haki za binadamu, na tumefanya haya yote ili tuwakumbushe watu kwamba alitoa familia yake yote kutangaza mambo yote ya kumpendeza Mungu" amesema. amefafanua.

Kumbukumbu ya kifo cha Mjukuu wa Mtume Imamu Husen hufanyika kila mwaka wailamu wakikusanyika wakifanya matendo ya kibinadamu yaliyokuwa yakifanywa na mtume huyo wakati wa enzi ya uhai wake.

Post a Comment

0 Comments