KIONGOZI wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka huu, Godfrey Mnzava amempongeza na kumshukuru Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa namna anavyoendelea kupambania afya za watanzania kwa kuboresha miundombinu ya sekta ya afya.
Mnzava ametoa pongezi hizo Julai 10,2024 wakati wa mbio za Mwenge wa Uhuru ulipofika katika hospitali ya wilaya ya Mkalama mkoani Singida, kuangalia vifaa tiba vilivyowezeshwa na Rais Dk. Samia.
"Mheshimiwa Rais Dk. Samia ameendelea kujenga miundombinu mingi sana ambayo ni rafiki na yakisasa kutolea huduma za afya, Hapa pia mmeletewa vifaa hivyo, tumekagua na kuona namna ambavyo vinaendelea kufanya kazi, kwa kweli tunampongeza na kumshukuru sana Rais Dk. Samia Suluhu Hassan
Amedokeza Rais ameyafanya hayo kwa lengo la kuhakikisha wananchi wanapata huduma za kibingwa na hawapati changamoto ya kuzifuata mbali na makazi yao na pia ameendelea kuboresha maslahi ya watumishi ili kuhakikisha tufikia malengo tulijiwekea kama taifa.
"Ameleta vifaa ambavyo vinasaidia kutafsiri changamoto za wagonjwa na mifumo ya hewa tiba kwa lengo la kuwasaidia watu wenye changamoto ya kupumua na upatikanaji wa hewa ndani ya miili yao ili waweze kupata unafuu," amesema.
Awali akiwasilisha taarifa fupi ya vifaa vya kisasa walivyovipata, Mganga Mfawidhi wa hospitali ya wilaya Mkalama, Dkt. Nicas Leonart amesema wanamshukuru Rais kwa kuwapatia vifaa ambavyo wanaamini vitawanufaisha wananchi wilayani Mkalama pamija na wilaya za Jirani ambazo ni Meatu, Mbulu, Manyara na Iramba.
Aidha, ameeleza serikali iliwapatia fedha za kujenga jengo la wagonjwa wa dharura kupitia mradi wa mapambano ya UVIKO-19 mwaka 2021. Amesema mradi huo, uligharimu sh millioni 300 kutoka serikali kuu huku katika mwaka 2023 hadi 2024 wakipokea vifaatiba vyenye thamani ya sh milioni 450.5.
Daktari Leonart amevitaja vifaa hivyo kuwa ni Portable x-ray, Oxygen Port, ventilators, Control ya Mfumo wa hewa tiba, Maniford Control (Mfumu wa hewa tiba), vitanda vya umeme vitano na vifaa vingine,"Vifaa hivi lengo lake ni kuboresha huduma kwa wagonjwa wa dharura," amesisitiza.
0 Comments