Baadhi ya Mafundi Rangi wa Mkoa wa Dodoma katika semina iliyoandaliwa na kampuni ya Utengenezaji , Uuzaji na Usambazaji wa Vifaa vya Ujenzi nchini ya KIBOKO PAINTS ambapo kampuni hiyo imetambulisha bidhaa yake mpya ya KIBOKO WALL PUTTY kwa mafundi hawa , sambamba na hilo KIBOKO PAINTS imemtambulisha Muigizaji Salim Ahmed ( Gabo Zigamba ) kama Balozi wake, utambulisho uliofanywa na Afisa Masoko Mkuu wa Kampuni ya KIBOKO PAINTS Bwn. Erhard Mlyansi ( pichani , picha ya 1 ) Julai , 20 , 2024 .
Mafundi wakiifanyia majaribio kwa kuipaka ubaoni bidhaa ya KIBOKO WALL PUTTY mbele ya wenzao ili kujionea ubora wake , Aidha Mafundi hawa wamezijaribu rangi za KIBOKO na kuyashuhudia maboresho makubwa ambayo kampuni imeyafanya katika rangi hizo.
Balozi wa KIBOKO PAINTS , Muigizaji Gabo Zigamba akiongea na Mafundi wa Dodoma kuhusu Bidhaa mpya ya KIBOKO WALL PUTTY.
Na Adery Masta.
Kampuni namba moja nchini kwa uuzaji wa Vifaa mbalimbali vya Ujenzi kama vile Mabati , Rangi n.k KIBOKO Paints, Imetambulisha Bidhaa yake mpya sokoni ya KIBOKO WALL PUTTY yenye Ubora wa hali ya juu kwa baadhi ya Mafundi Rangi wanaoishi na kufanya kazi mkoani Dodoma.
Julai, 20 , 2024 akizungumza baada ya Semina , Bwn. Hamidu Satara ambaye ni Afisa Mauzo wa kampuni, lakini pia Mkufunzi wa Semina hiyo amesema
" Kampuni ya KIBOKO PAINTS inafanya Semina hizi nchi nzima ambapo kwa upande wa Dar Es Salaam tumefanya Gongo la Mboto na maeneo yake ya karibu , Buguruni na maeneo yake ya karibu , Mbezi , Kariakoo , Mbagala na Kigamboni , Morogoro Mjini na Ifakara , kisha hapa Dodoma na Mkoa wa Mwanza unafuatia, Hakika niwapongeze mafundi wa Dodoma kwa muitikio wao mkubwa katika kuhudhuria semina hii na tumeelezana mengi kuhusu Bidhaa yetu mpya ya WALL PUTTY lakini pia na maboresho makubwa tuliyoyafanya katika rangi zetu " amesema Bw. Hamidu
Bi. Teddy Chinyoyo ni fundi aliyezungumza na Mwandishi Wetu Baada ya Semina hiyo ameipongeza kampuni ya KIBOKO PAINTS kwa kuileta sokoni KIBOKO WALL PUTTY yenye Ubora wa hali ya juu
"KIBOKO WALL PUTTY ni Bora sana ukiitumia hutopata gharama ya kununua material mengine tofauti ya kufanya Skimming , KIBOKO PAINTS wamefanya maboresho makubwa na kuja na Wall putty Bora kuliko nyingine zilizopo sokoni " amesema.
Aidha Bi. Teddy ameipongeza kampuni ya KIBOKO kwa kufanya maboresho makubwa katika rangi zake, kwa sasa ni miongoni mwa rangi bora zaidi sokoni.
0 Comments