Ticker

6/recent/ticker-posts

KATAMBI ATOA MAJIKO YA GESI KWA WAJUMBE WA BARAZA LA WAZEE MANISPAA YA SHINYANGA

Katibu wa mbunge Samwel Jackson akikabidhi jiko kwa Mwenyekiti wa baraza la ushauri la wazee manispaa ya Shinyanga Stephano Tano.

Na Mwandishi wetu - Malunde 1 blog

Mbunge wa jimbo la Shinyanga mjini Mhe. Patrobas Katambi ametoa majiko kwa baraza la wazee la ushauri wa manispaa ya Shinyanga katika kukabiliana na uharibifu wa mazingira na matumizi ya mikaa.

Majiko hayo yametolewa leo Julai 2, 2024 katika ofisi za Chama Cha Mapinduzi wilaya ya Shinyanga Mjini pamoja na utolewaji elimu ya matumizi ya majiko hayo.

Akizungumza wakati wa zoezi la ugawaji wa majiko hayo katibu wa mbunge Samwel Jackson amesema lengo la kutoa majiko hayo ni katika kuunga mkono suala la utunzaji wa mazingira kwa kuepuka ukataji wa miti kwaajili ya matumizi ya kupikia.

 Mhe. Katambi ametoa majiko haya 85 kwa baraza la ushauri la wazee wa manispaa ya Shinyanga yenye thamani ya shilingi Milioni 4,250,000/= kwa wazee kwa lengo la kutokomeza ukataji miti na kuepuka matumizi ya mkaa majumbani lakini pia kutoa elimu ya matumizi sahihi ya nishati safi ya kupikia kwa afya na utunzaji wa mazingira tunayoishi", amesema Samwel.

"Katika kuendeleza mapambano dhidi ya matumizi ya nishati chafu mpaka sasa Mhe. Mbunge Patrobas Katambi ameweza kutoa majiko ya gesi yapatayo 1,780 yenye thamani ya Shilingi Milioni 89 kwa wananchi 1,000 ndani ya manispaa ya Shinyanga lengo ni kuunga juhudi za Mheshimiwa Rais wetu hivyo ni lai yangu tuendelee kuyatunza majiko haya yaweze kutusaidia katika matumizi yetu ya kila siku", ameongeza Samwel.

Akitoa shukurani kwa niaba ya baraza hilo mara baada ya kupokea majiko hayo Mwenyekiti wa baraza la wazee wa manispaa ya Shinyanga Stephano Tano amesema watakwenda kuwa mabalozi wazuri katika kuhamasisha matumizi ya nishati safi kwenye jamii wanayoishi na kuepuka ukataji miti hovyo.

"Nitoe shukurani za dhati kwa niaba ya balaza la ushauri la wazee wa manispaa ya Shinyanga kwa kupatiwa majiko haya na pia tunamshukuru sana mheshimiwa mbunge wetu kwa kutukumbuka wazee na sisi kama washauri na viongozi kwenye kata mbalimbali tunazotoka kwenye maeneo yetu tutakwenda kihamasisha matumizi ya majiko haya kufuatia elimu hii ya matumizi ya majiko ya gesi tuliopatiwa siku ya leo", amesema Mzee Tano.

Katibu wa mbunge Samwel Jackson akizungumza wakati wa kugawa majiko hayo.

Katibu wa mbunge Samwel Jackson akizungumza wakati wa kugawa majiko hayo.
Katibu wa mbunge Samwel Jackson akikabidhi jiko kwa mmoja wa mjumbe wa baraza la ushauri la wazee manispaa ya Shinyanga.
Katibu wa mbunge Samwel Jackson akikabidhi jiko kwa mmoja wa mjumbe wa baraza la ushauri la wazee manispaa ya Shinyanga.

Afisa masoko kutoka ORYX Shinyanga Emmanuel Malisa akitoa elimu ya matumizi ya majiko ya gesi.
Baadhi ya majiko ya gesi yaliyotolewa.
Mwenyekiti wa baraza la wazee wa manispaa ya Shinyanga Stephano Tano akizungumza mara baada ya kupokea majiko hayo.
Mjumbe wa baraza la wazee la ushauri wa manispaa ya Shinyanga akitoa shukurani kwa Mheshimiwa Mbunge kwa kupatiwa majiko hayo.
Mjumbe wa baraza la wazee la ushauri wa manispaa ya Shinyanga akitoa shukrani kwa Mheshimiwa Mbunge kwa kupatiwa majiko hayo.

Mjumbe wa baraza la wazee la ushauri wa manispaa ya Shinyanga akitoa shukurani kwa Mheshimiwa Mbunge kwa kupatiwa majiko hayo.

Post a Comment

0 Comments