Watanzania wameshauria kujiunga na bima zinazotolewa na Benki ya CRDB ili ziwasaidie kuwakinga pale wanapokumbwa na majanga wakati wakitekeleza majukumu yao ya kila siku.
Wito huo umetolewa na Afisa kutoka Benki wa CRDB, Godfrey Tairo wakati akizungumza na waandishi wa Habari katika maonesho ya 48 ya kimataifa ya Biashara Sabasaba.
Amesema Benki hiyo inatoa Bima mbalimbali ikiwemo bima ya Afya ambayo inawalenga wanafamilia, wafanyakazi na wafanyabiashara.
Pia amesema wanatoa bima ya maisha ambayo inawalenga watu wote wakiwemo wafanyabiashara na vikundi ambapo katika vikundi hivyo wanachama watafaidika na bidhaa mpya ya ‘ Bima Vikundi’
Kadhalika Tairo amesema Benki hiyo inatoa Bima ya vyombo vya moto kama vike magari, Pikipiki, daladala na bajaji.
“Ukitaka kukata bima ya moto vitu tunavyobihitaji kutoka kwa mtaja ni kadi yake ya gari, kama akichagua bima kubwa atatakiwa aje na gari lake kabisa kwani lazima tulipige picha gari hilo kuhakikisha kuwa gari hilo lilikuwa katika hali nzuri, pia bima ndogo aje na kadi ya gari, kitambulisho cha nida au leseni yake au kitambulisho chochote kinachotambulika na serikali”
Tairo amesema Benki hiyo pia inatoa bima za majengo kama vile nyumba, shule na hospitali.
Kuhusu Bima ya maisha, Tairo amesema bima hiyo ipo katika pakage ya vikundi ambapo wanachama wanatakiwa kuanzia 10 na kuendelea.
“Hii inasaidia pale mwanachama akifariki au akifiwa na mtoto au mwenza tutamsaidia angalau wale wanaobaki kunakitu ambacho anaanzia nacho”
0 Comments