Ticker

6/recent/ticker-posts

CCM TANGA YAKABIDHI MILIONI 30 KUWASOMESHA MADEREVA WA DALADALA 600

MWENYEKITI wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Tanga Rajab Abdurhaman kulia akimkabidhi Fedha Taslimu milioni 30 Mkuu wa Mkoa wa Tanga Balozi Batilda Burian kwa ajili ya kuwawezesha madereva wa daladala 600 kwenda kusoma kwenye chuo cha Veta Tanga katikati aliyevaa suti nyeusi ni Mkuu wa Chuo cha Veta Tanga akkishuhudia.
MWENYEKITI wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Tanga Rajab Abdurhaman akizungumza wakati wa halfa hiyo kulia ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa huo Suleiman Sankwa
MKUU wa MKoa wa Tanga Balozi Batilda Burian akizungumza wakati wa halfa hiyo
KATIBU wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Tanga Suleiman Sankwa akizungumza wakati wa halfa hiyo kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga Rajab Abdurhaman

Na Oscar Assenga, TANGA

CHAMA cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Tanga kimewataka kimetoa kiasi cha Milioni 30 kwa ajili ya kugharamia masomo kwa ajili ya madereva wa daladala Jijini Tanga 600 katika chuo cha Veta ili waweze kukidhi vigezo vinavyotumika kuendesha vyombo vya usafiri.

Huku wakiwaonya madereva wanaofanya shughuli za usafirishaji katika mkoa huo kutokujihusisha na vitendo kutoa rushwa pale wanapokamatwa na askari wa usalama kutokana na makosa mbalimbali ya kukiuka sheria za usalama barabarani

Akizungumza wakati akikabidhi fedha hizo Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga Rajabu Abdurhaman alisema kwamba badala yake wahakikishe wanazingatia sheria za usalama barabarani na kuzifuata.

“Pamoja na yote niwasisitize madereva kuhakikisha tunafuata sheria za usalama barabarani kwa kuendesha vyombo vyetu vya moto tukiwa tumekidhi vigezo kwa kuwa na leseni”Alisema

Mwenyekiti huyo pia aliwataka madereva hao kuacha kuendesha vyombo vya moto kiholela bila kufuata sheria za usalama barabarani kwani kufanya hivyo wanachangia kuhatarisha maisha yao na abiria ambao wanakuwa wamepanda kwenye vyombo vyao.


“Lakini niwatake pia msiwe mahodari wa kulaumu askari wa usalama barabarani kwa sababu wamekiuka sheria za usalama badala yake wafuate utaratibu ili amani iendelee kutawala wanapokuwa wakiendesha vyombo vya moto.”Alisema Mwenyekiti huyo

“Ninaamini baada ya kupata mafunzo haya kwa mwezi mmoja kwenye katika chuo cha Veta kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi kitengo cha Usalama Barabarani yatawawezesha kuwaongezea elimu na kupata leseni ili kukidhi vigezo vya sheria vilivyowekwa”Alisema

Alisema lakini pia mafunzo hayo yatawaepusha na adha ya kukamatwa askari wa Jeshi la Polisi kitengo cha Usalama Barabarani kutokana na makosa mbalimbali ikiwemo ya kukosa leseni za udereva

Awali akizungumza katika halfa hiyo Mkuu wa Mkoa wa Tanga Balozi Batilda Burian alimshukuru Mwenyekiti huyo kwa kuwasaidia madereva hao kuweza kupata elimu katika chuo cha Veta itakayowawezesha kupata vigezo vya kuendesha vyombo vya moto.

Alisema kwamba viongozi wa madereva hao walifika ofisini kwake wakimpelekea malalamiko ya kuwa wanapokuwa katika shughuli zao wanakamatwa na polisi leseni zao zinachukuliwa na magari yao kuwekwa kituo cha polisi na wao kuwekwa ndani kutokana na kukosekana ukamilifu wa viwango ambavyo vinatakiwa ya kila mwenye leseni wawe wamekwenda chuo na kupata cheti cha kusomea.

“Nilipopata jambo hilo lilinisikitisha kidogo nikaona njia ya kuwasaidia nikaone nije kwako Mwenyekiti wetu wa Mkoa wa CCM kukueleza kilio hicho na baadae ukaona uwaite wakakuelezea shida zao na wewe ukaamu kulifanyia kazi sisi wengi tunahaidi lakini ahadi zetu zinaweza kuchukua mwaka au mwezi umehaidi na ahaidi yako imetilia kwa wakati tunakushurku sana”Alisema

“Mwenyekiti nikuhaidi kwamba tutaendelea kufanya kulingana na spidi yako na sisi kama serikali tutaiga kuhakikisha kila tunachokihaidia tunakitekeleza kwa wakati nah ii itapunguza kero na adha kubwa ambayo polisi walikuwa wakipata lakini madereva walikuwa wakipata na wengine kukosa ujira baada ya kukamatwa na gari kushikiliwa”Alisema

Naye kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Tanga (RTO) Inspekta Rajabu Ngumbi alisema kwamba kumekuwepo na idadi ya madereva ambao wamekuwa wakikamatwa kwa makosa ya kutokuwa na leseni ambalo ni suala muhimu kwao wanapokuwa barabarani.

Ngumbi alisema kwamba lazima madereva wahakikisha wanakidhi vigezo vya kuendesha vyombo vya moto kwa kuhakikisha wanapata elimu na baadae kukidhi kupata leseni ili kuweze kufanya kazi zao kwa ufanisi.

Post a Comment

0 Comments