Ticker

6/recent/ticker-posts

WIZARA YA KILIMO KUPITISHA RASMI MAZAO YAKE BANDARI YA TANGA.


Na Hamida Kamchalla, TANGA.

WIZARA ya Kilimo imetoa kibali rasmi cha kuanza kutumia bandari ya Tanga kuwa njia ya kusafirishia mazao yote ya kilimo kutokana na maboresho makubwa yaliyofanywa na kuwa na viwango vinavyostahili.

Mkuu wa Mkoa wa Tanga Balozi, Dkt. Batilda Buriani ameyaeleza hayo kwenye kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani, yaliyofanyika kata ya Pande, jijini Tanga.


Dkt. Buriani amebainisha kwamba maboresho makubwa yaliyofanywa katika bandari hiyo yameendelea kupanua wigo wa usafirishaji wa mizigo kwani mizigo inayoingia imeongezeka kwa kiasi kikubwa.


"Kwasasa bandari ya Tanga siyo saidizi bali ni bandari yenye viwango vyote vinavyostahili na inayojitegemea kwa nafasi yake,


"Wenzetu wa Wizara walikuja wakakagua bandari na wametupa cheti rasmi kwamba sasa bandari yetu itatumika kusafirisha mazao ya kilimo, hivyo ili vitu vyote viende sawa kunatakiwa kuwe na uratibu mzuri" amesema.


Aidha mkuu huyo amepongeza usimamizi wa Simba Bingwa na makampuni yake kwa kuendelea kusimama mikataba ya usafirishaji wa majini kwa kuzingatia utoaji wa taarifa kuhusu bidhaa zinazosafirishwa ili kuepuka mchanganyiko wa kemikali na bidhaa nyingine.


Dkt. Buriani amesema upo mkataba ambao unazungumzia kuhusu usafirishaji wa bidhaa zenye kemikali zenye madhara na hilo linatekelezwa na kampuni hiyo ambapo wanapotaka kusafirisha ni lazima watoe taarifa kwa bandari.



"Hii inasaidia kutoleta madhara wakati wa upakuaji na pia kuwa na umakini zaidi, lakini kwa hili niwapongeze sana kwasababu wameonesha kusimama kidedea kutumia bandari ya Tanga" amesema.


Lakini pia amehimiza kuwa ili kutumza mazingira na kuondokana na mabadiliko ya tabianchi, kila mmoja anapaswa kutuma mazingira kwa kupanda miti haijalishi hata kwa wazee kwani itasaidia vizazi vyao kwa baadaye.



Mbali na hayo mkuu huyo amezindua mradi wa upandaji miti wa 'miti 23' unaorndeshwa na kampuni hiyo.


Naye Mkurugenzi wa Simba Solutions Ally Dewji amesema kampuni hiyo imeanzisha kitengo cha Simba Terminajs kwa lengo la kufanya utafiti wa soko ili kuwekeza katika tehama za mtiririko wa ugavi.


"Utafiti wetu ulionesha kwamba kutakuwa na mapinduzi makubwa katika uchumi wa Mkoa wa Tanga, hususani mnyororo mzima wa thamani kupitia mshorona mpya ambayo kwa sasa unajulikana kama Tanga Korido" amesema.


Dewji amebainisha kwamba takwimu zinaonesha mwaka jana bandari ya Tanga ilihudumia meli 19 ambapo meli 5 zilisimamiwa kikamilifu na kitengo cha Simba Terminals ambayo ni sawa na asilimia 26 ya meli zote zilizohudumiwa bandarini hapo.


"Kuendelea kupokea meli kupitia bandari hii kumeleta matokeo chanya ya uchumi katika Mkoa wa Tanga na nchi kwa ujumla, ikiwa ni pamoja na ukuzaji wa ajira kwa vijana wa Kitanzania,


"Kwa kawaida kila tunapokuwa na meli bandarini tumekuwa tukiajiri vijana kuanzia 250 hadi 300 Kwa ajili ya kutoa huduma mbalimbali" amesema.


Pia Dewji amebainisha kwamba wanayo furaha kubwa kwa kujua kampuni imeshiriki katika maisha yao kufungua tena bandari ya Tanga, lakini pia wanayo mengi ambayo wamewekeza katika Mkoa huo.


Hata hivyo amesema, katika kuadhimisha kilele cha siku ya Mazingira, kampuni hiyo imeadhimia kujenga Tanki pamoja na kisima kirefu cha maji katika shule ya sekondari Pande ambayo wameonesha ina tatizo kubwa la upatikanaji wa maji.

Post a Comment

0 Comments