Mfugaji mkubwa wa nguruwe anayemiliki mradi wa Kijiji cha Nguruwe Dodoma Simon Mkondya almaarufu MR MANGURUWE ametoa tamko akijibu malalamiko yaliyotolewa na mmoja kati ya wawekezaji kwenye mradi wake, MR MWANYA aliyeibuka na kumshukia vikali kufuatia tamko lake la kutaka kumuoa Shilole.
Mr Mwanya amenukuliwa akisema hawezi kukubali kuona mwekezaji huyo akiacha kutunza fedha za watu waliowekeza kwake na kuanza kujihusisha na mapenzi na mastaa.
Akimjibu Mr Mwanya,Mr Manguruwe amesema hawezi kupuuza kilichosemwa na mchekeshaji huyo lakini hana elimu ya uchumi ya kutosha na kwamba maisha yake binafsi hayahusiani na miradi yake.
"Tunadhani aidha hana elimu ya biashara au uchumi au ameamua kutumia comedy kwenye biashara," amesema Mr Manguruwe.
Ameongeza kwa kuwatoa wasiwasi wateja wake kwamba miradi yote inaendelea vizuri na hakuna kitakachoharibika.
Wasiliana na Mr Manguruwe kwa simu namba Namba +255763755755
MR MANGURUWE ATAKA KUMUOA SHILOLE
Soma pia
0 Comments