Ticker

6/recent/ticker-posts

RC CHALAMILA USO KWA USO NA WANAFUNZI WA DUCE

-Amshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa uwekezaji mkubwa katika nyanja za elimu hapa nchini-Awataka wanafunzi kutokata tamaa, wanayo nafasi kubwa ya kubadili maisha yao.

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo Juni 6,2024 amefanya ziara katika chuo Kikuu kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) ikiwa ni muendelezo wa ziara zake katika vyuo vikuu vya Mkoa huo.

RC Chalamila akiwa katika Chuo hicho amepata wasaa wa kuongea na menejimenti ya chuo hicho na baadae kukutana na wanafunzi katika Ukumbi wa mikutano.

Akiongea na wanafunzi hao amewataka kuachana na utamaduni wa kulalamika, badala yake wawe mabalozi wazuri wa Serikali " Rais Dkt Samia Suluhu Hassan amekuwa kinara wa uwekezaji mkubwa katika nyanja za elimu katika chuo hiki tayari ameshatoa pesa si chini ya Bilioni 19, kwa ajili ya kufanya maboresho ya miundombinu ya Chuo hicho" Alisema RC Chalamila

Aidha RC Chalamila amesema kwa upande wa mikopo ya vyuo vikuu Mhe Rais ameongeza fedha katika bodi ya mikopo ya elimu ya juu kwa ajiri ya kutanua wigo wa wanufaika wa mikopo, hivyo wanafunzi watumie vizuri fursa hiyo.

Sanjari na hilo Mhe Albert Chalamila ameiagiza Bodi ya Mikopo Kuweka kambi katika chuo hicho ili kuwasaidia wanafunzi kufuata taratibu zote za kuomba mikopo bila kukosea ili unapokuja Wakati wa kutolewa mikopo pasiwe na malalamiko ya mwanafunzi kukosa mkopo kwa kutokana na kukosea wakati wa kujaza fomu za maombi.

Kwa upande wa Makamu Mkuu wa Chuo Prof Stephen Maluka Serikali ya Rais Dkt Samia tayari imeshatoa kiasi cha pesa sio chini ya Bilioni 19 ambazo zinakwenda kujenga majengo mawili ya kisasa ya Ghorofa 5, viwanja vya kisasa vya michezo hususani kwa wenye uhitaji, sweeming pool, na ukarabati wa Hosteli pale Mbagala pamoja na Internet ambayo tayari imeshawekwa katika maktaba chuoni hapo hivyo Rais Dkt Samia anastahili pongezi kubwa sana

Mwisho Mhe Albert Chalamila aliambatana na wataalam na Viongozi mbalimbali kutoka Serikalini na chama wakiwemo Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Temeke, wataalam kutoka NHIF, NACTVET, TCU, NIDA pamoja na Bodi ya Mikopo 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe Albert Chalamila akizungumza na Wanafunzi wa Chuo Kishiriki Cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) (hawapo pichani) mara baada ya kufanya ziara Chuoni hapo kwaajili ya kuzungumza na wanafunzi hao leo Juni 06, 2024 Jijini Dar es Salaam
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe Albert Chalamila akizungumza na Wanafunzi wa Chuo Kishiriki Cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) (hawapo pichani) mara baada ya kufanya ziara Chuoni hapo kwaajili ya kuzungumza na wanafunzi hao leo Juni 06, 2024 Jijini Dar es Salaam
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe Albert Chalamila akizungumza na Wanafunzi wa Chuo Kishiriki Cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) (hawapo pichani) mara baada ya kufanya ziara Chuoni hapo kwaajili ya kuzungumza na wanafunzi hao leo Juni 06, 2024 Jijini Dar es Salaam
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe Albert Chalamila akisisitiza jambo wakati akizungumza na Wanafunzi wa Chuo Kishiriki Cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) (hawapo pichani) mara baada ya kufanya ziara Chuoni hapo kwaajili ya kuzungumza na wanafunzi hao leo Juni 06, 2024 Jijini Dar es Salaam
Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mhe Sixtus Mapunda akizungumza na wanafunzi wa Chuo Kishiriki Cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) (hawapo pichani) wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe Albert Chalamila Chuoni hapo kwaajili ya kuzungumza na wanafunzi hao leo Juni 06, 2024 Jijini Dar es Salaam
Rasi wa Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE), Prof. Stephen Oswald Maluka akizungumza na wanafunzi wa Chuo Kishiriki Cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) (hawapo pichani) wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe Albert Chalamila Chuoni hapo kwaajili ya kuzungumza na wanafunzi hao leo Juni 06, 2024 Jijini Dar es Salaam
Rasi wa Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE), Prof. Stephen Oswald Maluka akizungumza na wanafunzi wa Chuo Kishiriki Cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) (hawapo pichani) wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe Albert Chalamila Chuoni hapo kwaajili ya kuzungumza na wanafunzi hao leo Juni 06, 2024 Jijini Dar es Salaam
Rasi wa Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE), Prof. Stephen Oswald Maluka akisisitiza jambo wakati akizungumza na wanafunzi wa Chuo Kishiriki Cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) (hawapo pichani) wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe Albert Chalamila Chuoni hapo kwaajili ya kuzungumza na wanafunzi hao leo Juni 06, 2024 Jijini Dar es Salaam
Naibu Rasi-Taaluma, Utafiti na Ushauri Elekezi, Chuo Kishiriki Cha Elimu Dar es Salaam (DUCE), Dkt. Christina Raphael akizungumza na wanafunzi wa Chuo Kishiriki Cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) (hawapo pichani) wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe Albert Chalamila Chuoni hapo kwaajili ya kuzungumza na wanafunzi hao leo Juni 06, 2024 Jijini Dar es Salaam
Naibu Rasi-Taaluma, Utafiti na Ushauri Elekezi, Chuo Kishiriki Cha Elimu Dar es Salaam (DUCE), Dkt. Christina Raphael akizungumza na wanafunzi wa Chuo Kishiriki Cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) (hawapo pichani) wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe Albert Chalamila Chuoni hapo kwaajili ya kuzungumza na wanafunzi hao leo Juni 06, 2024 Jijini Dar es Salaam.
Naibu Rasi (Utawala, Fedha na Mipango) Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) Dkt.Method Samwel akizungumza na wanafunzi wa Chuo Kishiriki Cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) (hawapo pichani) wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe Albert Chalamila Chuoni hapo kwaajili ya kuzungumza na wanafunzi hao leo Juni 06, 2024 Jijini Dar es Salaam.
Wanafunzi wa Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe Albert Chalamila mara baada ya kufanya ziara Chuoni hapo leo Juni 06, 2024 Jijini Dar es Salaam
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe Albert Chalamila akiwa kwenye picha ya pamoja na wadau mbalimbali wa elimu mara baada ya kufanya ziara katika Chuo Kishiriki Cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) kwaajili ya kuzungumza na wanafunzi wa Chuoni hapo leo Juni 06, 2024 Jijini Dar es Salaam

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

Post a Comment

0 Comments