Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Korea Mhe. Yoon Suk Yeol wakati wakishuhudia Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji pamoja na Waziri wa Biashara wa Korea Inkyo Cheong wakisaini Tamko la Pamoja kuhusu Uanzishwaji wa Majadiliano juu ya Mkataba wa Ushirikiano Kiuchumi. Hafla ya utiaji saini imefanyika katika Ikulu nchini humo tarehe 02 Juni, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan pamoja na Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Korea Mhe. Yoon Suk Yeol wameshuhudia utiaji saini Mkataba (1) Hati za Makubaliano (2) na Tamko la Pamoja la kuanzisha Mkataba wa Ushirikiano Kiuchumi (1) kwenye hafla iliyofanyika Ikulu nchini humo tarehe 02 Juni, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Korea Mhe. Yoon Suk Yeol wakati wakishuhudia Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba pamoja na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Uchumi na Fedha (Jamhuri ya Korea) Choi Sang Mok wakisaini Mkataba wa Ushirikiano kati ya Tanzania na Korea kuhusu Mkopo unaotolewa na Mfuko wa Ushirikiano wa Maendeleo ya Uchumi wa Serikali ya Korea (Economic Development Cooperation Fund-EDCF). Hafla ya utiaji saini imefanyika katika Ikulu nchini humo tarehe 02 Juni, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Korea Mhe. Yoon Suk Yeol wakati wakishuhudia Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba pamoja na Waziri wa Biashara wa Korea Inkyo Cheong wakibadilishana Hati ya Makubaliano kati ya Wizara ya Madini ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Wizara ya Biashara, Viwanda na Nishati ya Jamhuri ya Korea kuhusu Ushirikiano katika Madini ya Kimkakati. Hafla ya utiaji saini imefanyika katika Ikulu nchini humo tarehe 02 Juni, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Korea Mhe. Yoon Suk Yeol wakati wakishuhudia Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba pamoja na Waziri wa Uvuvi na masuala ya Bahari kutoka Jamhuri ya Korea Kang Do-Hyung wakisaini Hati baina ya nchi mbili kuhusu Ushirikiano katika maendeleo ya Uchumi wa Buluu. Hafla ya utiaji saini imefanyika katika Ikulu nchini humo tarehe 02 Juni, 2024.
0 Comments