Ticker

6/recent/ticker-posts

VIRIDIUM YATOA ELIMU YA MATUMIZI YA MKAA MWEUPE KWENYE KONGAMANO LA MAZINGIRA

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

Katika kuunga jitihada na juhudi ya serikali katika kuhakikisha matumizi ya nishati safi ya kupikia inapatikana kwa wananchi kwa gharama nafuu,Kampuni ya Viridium Tanzania Limited imeonesha bidhaa yake ya mkaa mweupe katika kongamano la mazingira Jijini Dar es Salaam ambapo imelenga kusaidia wananchi kuachana na matumizi ya kuni na mkaa ili kudhibiti madhara ya kiafya.

Akizungumza katika Kongamano hilo,leo Mei 31,2024 Afisa Masoko wa Viridium Tanzania Limited Bw.Abuu Habibu amesema mkaa wao ni nishati Safi ya kupikia ambao hauna madhara yanayotokana na moshi kwani hautumii miti bali unatengenezwa na majani maalumu wanayoyalima katika shamba lao eneo la Kidamali Mkoani Iringa.

Aidha amesema mkaa huo unafaida kubwa katika mazingira kwani hautumii mti bali unatumia majani pekee pia unakaa kwa muda mrefu pia kwa vipande vitano unatosha kupikia chakula kulingana na idadi ya watu katika familia.

"Mkaa wetu unakaa sana jikoni na unakaa vizuri, unatumia muda mrefu ukiwa unawaka"amesema Habibu

Pamoja na hayo Habibu ameeleza kuwa mkaa wao mweupe hautoi moshi wala hauna madhara kwani hata Taasisi ya biashara nchini umeshawahi kupima nakujiridhisha kuwa hauna madhara yanayotokana na moshi.

"Mkaa wenyewe hauna madhara kwani tunatumia majani ambayo hata ng'ombe anakula"Bw.Habibu ameeleza.

Vilevile Bw. Habibu amesema nishati hiyo ya mkaa mweupe inapatikana kote nchini kwa mtu au taasisi ambayo itapenda kutumia bidhaa yao anatakiwa kutoa oda.

Post a Comment

0 Comments