Wanakijiji wa kijiji cha Chole wilayani Momba wametakiwa kuachana na kuuza mazao ya chakula ili kujikinga na njaa kipindi cha kilimo.
Kauli hiyo imetolewa Mei 13, 2024 na Koplo James Chitukulu wakati akizungumza na wanakijiji hao kwa lengo la kuwajengea uelewa kuhusu umuhimu wa kutunza mazao ya chakula ili kujiepusha na janga la njaa.
Koplo James alisema kuwa, acheni kuuza chakula chote kwani kufanya hivyo mnajitengenezea mazingira magumu kipindi cha kilimo ambapo mnapelekea kuingia kwenye madeni na mikopo kausha damu ambayo inaleta ugomvi usiokuwa na mwisho katika familia zenu.
"Wanaume wenzangu acheni kuuza mazao na kwenda kunywa pombe na kuongeza mke huku ukiitelekeza familia yako mnatakiwa kusomesha watoto na kufanya maendeleo katika maisha yenu ya kila siku, shirikiana na mwenza wako ili mpige hatua za kimaendeleo kila mwaka wa mavuno kwa manufaa ya maisha na maendeleo ya familia zenu " alisisitiza Koplo James
Koplo Jamea aliwataka wanakijiji hao kuendelea kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu wa mazao na mifugo yao ili ziwezekushughulikiwa kwa haraka ikiwa ni pamoja na kuwafikisha mahakamani ili iwe fundisho kwa watu wenye tabia kama hizo.
0 Comments