Ticker

6/recent/ticker-posts

RAIS SAMIA AHUTUBIA KATIKA MAADHIMISHO YA MIAKA 20 YA BARAZA LA AMANI NA USALAMA LA UMOJA WA AFRIKA (AU) JIJINI DAR ES SALAAM

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika (AU) akihutubia viongozi mbalimbali wakati wa Maadhimisho ya miaka 20 ya Baraza hilo katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam tarehe 25 Mei, 2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea Tuzo Maalum kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AU) Mhe. Moussa Faki Mahamat wakati wa Maadhimisho ya miaka 20 ya Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika (AU) yaliyofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam tarehe 25 Mei, 2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Amani na Usalama akimvalisha Nishani ya Heshima Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa Awamu ya Nne Mhe. Dkt. Jakaya Kikwete kwa kutambua mchango wake katika eneo la Amani na Usalama Barani Afrika wakati wa Maadhimisho ya miaka 20 ya Baraza hilo. Maadhimisho hayo yalifanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam tarehe 25 Mei, 2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Amani na Usalama akimvalisha Nishani ya Heshima Rais Mstaafu wa Nigeria Olusegun Obasanjo kwa kutambua mchango wake katika eneo la Amani na Usalama Barani Afrika wakati wa Maadhimisho ya miaka 20 ya Baraza hilo. Maadhimisho hayo yalifanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam tarehe 25 Mei, 2024. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Amani na Usalama akimvalisha Nishani ya Heshima Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AU) Mhe. Moussa Faki Mahamat kwa kutambua mchango wake katika eneo la Amani na Usalama Barani Afrika wakati wa Maadhimisho ya miaka 20 ya Baraza hilo. Maadhimisho hayo yalifanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam tarehe 25 Mei, 2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Amani na Usalama akimvalisha Nishani ya Heshima Rais Mstaafu wa Burundi Mhe. Domitien Ndayizeye kwa kutambua mchango wake katika eneo la Amani na Usalama Barani Afrika wakati wa Maadhimisho ya miaka 20 ya Baraza hilo. Maadhimisho hayo yalifanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam tarehe 25 Mei, 2024.

Post a Comment

0 Comments