Na Mwandishi wetu, Hanang'
SHIRIKA la Amref Tanzania na shirika la Marekani la kudhibiti na kuzuia magonjwa (CDC) limewanufaisha wanafunzi 3,000 wa shule za msingi na sekondari wilaya ya Hanang' mkoani Manyara, baada ya kuwajengea miundombinu ya kudhibiti magonjwa ya milipuko.
Mashirika hayo yamewanufaisha wanafunzi hao kwa kuzindua maeneo ya kunawa mikono na kukarabati vyoo.
Mkurugenzi mkazi wa Amref Tanzania, Dkt Florence Temu amesisiza umuhimu wa mbinu jumuishi za kuimarisha magonjwa ya mlipuko katika jamii kupitia ufuatliaji wa huduma za maji na usafi wa mazingira.
Amesema maendeleo makubwa yaliyopatikana katika ufuatiliiaji wa mapema na kukabiliana na vitisho vya afya ya umma katia kanda hiyo hasa magonjwa ya mlipuko,
Dkt Temu amesema ushirikiano kati ya Amref Tanzania na Kituo cha serikali ya Marekani (CDC) Tanzania, umekuwa na mchango mkubwa katika kutoa ushauri na uhamasishaji katika uboreshaji wa huduma za maji na usafiwa mazingira hivyo kusababisha kuzuia magonjwa ya kuambukiza katika kanda.
Mkuu wa usalama na udhibiti wa uchafuzi wa mazingira Wizara ya Afya, Dkt Honestus Anicetus ameipongeza serikali ya Tanzania, kituo cha serikali ya Marekani cha kudhibiti na kuzuia magonjwa (CDC) Tanzania na Amref Tanzania kwa juhudi zao za kuunga mkono serikali kuimarisha mfumo wa ufuatiliaji wa mazingira.
Dkt Anicetus amesema serikali imeboresha Sekta ya afya kupitia miradi mbalimbali ya afya nchini kwa uwajibikaji wa utunzaji wa maeneo hayo na
Amesisitiza haja ya kuchukuliwa hatua za kisheria kwa yeyote atakayesababisha uharibifu au uzembe.
Mkurugenzi wa Kitengo cha ulinzi wa afya, katika kituo cha serikali ya Marekani cha kudhibiti na kuzuia magonjwa (CDC) Tanzania, Dk Wangeci Gatei amesema dhamira ya CDC Tanzania kuimarisha mbinu za kuzuia maambukizi ya magonjwa ya mlipuko Tanzania kupitia juhudi za ushirikiano na serikali na washirika wa ndani.
Amesema lengo ni kuisaidia Tanzania katika kuzingatia kanuni za kimataifa za afya (2005) kupitia malengo ya Global Health Security Agenda (GHSA) 2024.
Mwanafunzi wa shule ya sekondari Ganana, Emmanuel Amani amesema wanashukuru kwa msaada huo utakaowanufaisha wao.
Ofisa afya wa mkoa wa Manyara, Sultan Mwabulambo amepongeza hatua hiyo kwani umuhimu wake ni mkubwa kwa wanafunzi wa maeneo hayo ambayo yalikumbwa na maafa mwishoni mwa mwaka jana.
Mwakilishi wa mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Hanang' Dk Mohamed Kodi amesema miundombinu hiyo itakuwa kichocheo kikubwa kwa wanafunzi hao kupata elimu kwenye mazingira rafiki.
Hafla ya makabidhiano hayo imehudhuriwa na mwakilishi wa Wizara ya Afya, kituo cha Serikali ya Marekani (CDC) Tanzania, Amref Tanzania na viongozi wa Serikali za mitaa, wahudumu wa afya ya jamii, walimu na wanafunzi.
0 Comments