Mbunge wa Jimbo la Kishapu Mkoani Shinyanga Mhe. Boniphace Butondo leo Mei 4,2024 amezindua ligi ya Shagy Cup katika viwanja vya shule ya msingi Lubaga kata ya Kishapu inayohusisha timu 16 zilizoko ndani na nje ya jimbo hilo.
Mhe.Butondo ambaye ndiye mdhamini mkuu wa Shagy Cup aliyetoa jezi na mipira kwa timu zote 16 akizungumza wakati wa ufunguzi amesema washiriki wote watambue kuwa hiyo ni fursa adhimu isoyotakiwa kupotezwa kwani michezo inatoa ajira,inajenga undugu,umoja na mshikamano.
"Nimpongeze sana mwandaaji wa ligi Shagy ndugu yangu Elias Shagg amekuwa ni kijana wa mfano mpaka jioni ya leo kutukutanisha hapa, nitoe rai kwa vijana wengine tusikae vijiweni kupoteza muda,usiwaze kufanya uhalifu ili ujipatie kipato,usiwaze mabaya kwa watu wengine cha zaidi ni kufanya kazi na tumpe ushirikiano kijana mwenzetu kwa kujiunga na timu mbalimbali kwani mpira kwa sasa ni ajira", ameongeza Mhe. Butondo.
Aidha ameongeza kuwa serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Hassan imejitoa kikamilifu kusaidia sekta ya michezo hivyo mbunge na diwani wanaowajibu mkubwa wa kuhakikisha wanasimamia kutekeleza ilani ya Chama Cha Mapinduzi.
"Ndugu zangu si tu michezo mmejionea wenyewe serikali inavyojitahidi kuboresha huduma mbalimbali za jamii ikiwemo ukarabati wa majengo na ujenzi wa shule, mmesogezewa huduma ya umeme,ukarabati wa miundombunu ya barabara,na hata sasa mpango wa serikali yenu ni kuwasogezea huduma ya maji safi" ,ameongeza Mhe. Butondo.
Aidha amewataka waamuzi wa ligi hiyo watende haki kwa kuzingatia sheria 17 za soka ikiwa wao wananafasi kubwa ya kuufanya mchezo kuwa mzuri ama mbaya huku akiwakumbusha wachezaji kuzingatia upendo,furaha na amani wakati wa mchezo na sio ugomvi na kutoleana maneno mabaya.
Diwani wa Kata ya Kishapu Mhe.Joel Ndettoson amempongeza Mbunge wa Kishapu kwa kudhamini mchezo huo na Shagy kwa kuanzisha ligi hiyo itakayochezewa kwenye viwanja vya michezo Shule ya msingi Lubaga huku akiongeza kuwa michezo siku zote ni ajira,ni furaha pamoja na kutengeneza afya bora na imara.
Timu zilizocheza leo ni Unyanyembe Fc na Lubaga Fc huku Unyangembe ikiibuka mshindi wa bao 1-0 kipindi cha kwanza dhidi ya Lubaga Fc na kadi nyekundu kutolewa kwa mchezaji wa Lubaga kipindi cha pili na kadi ya njano zikitolewa 2 kwa Unyanyembe Fc na 1 kwa Lubaga Fc na kesho Mei 5 watacheza Talent Fc dhidi ya Ikonda Fc katika viwanja hivyo hivyo.
Timu zinazoshiriki Ligi ya Shagy ni pamoja na Mwakasumbi,Polis Kishapu,Mwataga,Farmer,Ngundangari,Mwamashele,Ashanti,Talents,Barcelona,Maganzo,Madrid Mwanulu,Ikonda,Unyanyembe,Lubaga,Igwata pamoja na Bodaboda Fc.
Mbunge wa jimbo la Kishapu Mkoani Shinyanga Mhe. Boniphace Butondo na mdhamini mkuu wa ligi ya Shagy akizungumza wakati akizundua ligi hiyo leo Mei,4,2024 katika viwanja vya shule ya msingi Lubaga wilayani Kishapu
Mbunge wa jimbo la Kishapu Mkoani Shinyanga Mhe.Boniphace Butondo na mdhamini mkuu wa ligi ya Shagy akizungumza wakati akizundua ligi hiyo leo Mei,4,2024 katika viwanja vya shule ya msingi Lubaga wilayani Kishapu
Mwandaaji wa Shagy Ligi Bw. Shagy Elias akifurahia ufadhili wa Mbunge wa Kishapu Mhe. Boniphace Butondo wakati akikabidhi jezi na mipira kwa timu zote 16 zinazoshiriki ligi hiyo iliyozinduliwa leo Mei,4,2024 na Mbunge huyo katika viwanja vya shule ya msingi Lubaga.
Kushoto Mhe.Mbunge wa Kishapu mkoani Shinyanga Boniphace Butondo,Mwamuzi Bw.Masesa Kuzenza, Diwani wa Kata Kishapu Joel Ndettoson,na wa mwisho kulia ni katibu wa mbunge Bw.Godfrey Mbussa wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ta uzinduzi wa Shagy ligi iliyozinduliwa Mei,5,2024 na Mbunge katika viwanja vya shule ya msingi Lubaga
Diwani wa Kata ya Kishapu Joel Ndettoson akizungumza katika uzinduzi wa ligi ya Shagy iliyozinduliwa leo Mei,5,2024 na Mbunge wa jimbo la Kishapu Mhe.Boniphace Butondo.
Mbunge wa jimbo la Kishapu Mkoani Shinyanga Mhe.Boniphace Butondo akikabidhi jezi na mpira kwa mwakilishi wa timu ya Bodaboda mei,5,2024 akiwa mdhamini mkuu wa ligi ya Shagy aliyoizundua hii leo katika viwanja vya shule ya msingi Lubaga kata ya Kishapu.
Picha ya pamoja ya Mbunge wa jimbo la Kishapu mkoani Shinyanga Mhe. Boniphace Butondo ,diwani kata ya Kishapu na polisi Kata,viongozi mbalimbali pamoja na wachezaji wa timu ya Unyanyembe waliochuana vikali na Lubaga Fc wakitoka na ushindi wa bao 1-0 katika viwanja vya shule ya msingi Lubaga wilayani humo kwenye uzinduzi wa Shagy ligi.
Picha ya pamoja ya Mbunge wa jimbo la Kishapu mkoani Shinyanga Mhe. Boniphace Butondo ,diwani kata ya Kishapu na polisi Kata pamoja na wachezaji wa timu ya Lubaga waliochuana na Unyanyembe wakipokea kichapo cha bao 1-0 katika viwanja vya shule ya msingi Lubaga wilayani humo kwenye uzinduzi wa Shagy ligi.
Mashabiki wakifuatilia mechi kati ya Lubaga Fc na Unyanyembe Fc Ligi ya Shagy iliyozinduliwa leo Mei,5,2024 na Mbunge wa Kishapu Mhe. Boniphace Butondo akiwa pia mdhamini mkuu wa ligi hiyo aliyetoa mipira na jezi kwa timu zote 16 katika viwanja vya shule ya msingi Lubaga wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga.
0 Comments