Ticker

6/recent/ticker-posts

MAENDELEO BANK PLC YAZINDUA TAWI JIPYA MBAGALA ZAKHIEM

MKUU wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Albert Chalamila leo Mei 22,2024 amefungua rasmi tawi jipya la Benki ya Maendeleo Mbagala Zakhiem Wilaya ya Temeke Jijini humo.

Akiongea wakati wa hafla ya ufunguzi wa Benki hiyo ameipongeza menegimenti ya Maendeleo Benki kwa uwekezaji mkubwa na namna walivyojipanga kutoa huduma bora za kibenk katika Mkoa wa Dar es salaam hususani kwa wakazi wa Mbagala.

Mhe Chalamila amesema Benk ni Kichocheo cha uchumi wa mtu mmojammoja na taifa kwa ujumla ambapo amewataka wafanyakazi wa benk hiyo kufanya kazi kwa weledi na kuzingatia maadili ya kibenk ili kuwezesha kukua kwa benk hiyo

“Chakula cha benk ni Mikopo hivyo unapochukua mkopo hakikisha unakuwa na nidhamu ya kutosha ya urejeshaji” Alisema RC Chalamila

Aidha RC Chalamila amesema serikali inaendelea kuweka mazingira bora na Rafiki ya uwekezaji katika sekta ya Benk ndio maana leo tunashuhudia maendeleo benk wakiongeza tawi jipya katika eneo hili la mbagala huu ni uthibitisho wa sera nzuri zilizowekwa na Serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania chini ya Rais mahiri Dkt Samia Suluhu Hassan.

Vilevile Mkuu wa Mkoa ameihakikishia benki hiyo usalama wa kutosha wakati wote na dhamila ya serikali ya mkoa ni kuweka kituo kikubwa cha polisi Mbagala ikiwa ni moja ya maandalizi ya kuelekea kufanya biashara Saa 24 ili kukuza uchumi wa wanambagala na Taifa kwa Ujumla

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Maendeleo Bank PLC Dkt. Ibrahim Mwangalaba
amesema benki imezindua huduma zake mbili za Mikopo ya Nufaika na Rasimisha Ardhi ikiwa ni mwendelezo wa hadhima yake ya kumuinua mfanyabiashara mdogo.

Amesema kupitia mkopo huu wa Nufaika Biashara mteja anaweza kukopa mpaka million 10 kwa kutumia Hati ya mauziano kwa ajili ya kukuza mtaji wa biashara yake huku ikimpa nafasi pia ya kurasimisha ardhi na kupata Hati miliki kupitia mkopo wa Rasimisha Ardhi.


"Mikopo hii ya Nufaika ni mahususi kwa wateja wadogo waliopo kwenye sekta isiyo rasmi kama vile Mama Lishe, Viosk, Mighawa midogo nk. Wateja hawa kama walivyo wamachinga wana changamoto kubwa ya kukubalika kwenye taasisi za fedha kutokana kukosa nyaraka rasmi za biashara zikiwemo utunzaji sahihi wa taarifa za biashara na dhamana zilizo rasmi kama hati ya nyumba au leseni ya Makazi.

Post a Comment

0 Comments