Ticker

6/recent/ticker-posts

TAMISEMI, WIZARA YA ELIMU KUWAKWAMUA WANAFUNZI WALIOKWAMA NA MAFURIKO

KUTOKANA na hali ya mafuriko yanayoendelea, Ofisi ya Rais-TAMISEMI na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia zimekubaliana namna ya kuwasaidia wanafunzi waliokwa kuendelea na masomo ili waendelee na masomo.

Akizungumza leo mara baada ya kikoa kilichowakutanisha mawaziri na walaamu wa wizara hizo mbili, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mohamed Nchengerwa amesema kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha kuna baadhi ya wanafunzi wameshindwa kuendelea na masomo kutokana na changamoto ya mafuriko.

“Kutokana na hali ya mfuriko yanayoendelea nchini, mimi na mwenzangu wa wizara ya elimu (Profesa Adolf Mkenda) tumekubaliana sasa tunakazi ya kuja na mpango wa muda mfupi na muda mrefu ambao utawawezesha vijana wetu wanaosoma shule mbalimbali ambao leo hii wamekwama kuendela na masomo kwasababu ya majanga ya mafuriki yanayoendelea kote nchini hususani katika mikoa ya Pwani, Morogoro, Katavi na mikoa ya kaskazini na kusini.”

Amesema katika kutekeleza hilo wizara zimewaelekeza wataalamu kutoka wizara hizo kwenda nchi nzima kufanya tathimini na kujiridhisha kutokana na uharibifu mkubwa wa miundombinu ya shule uliochangiwa na mafuruki.

“Tutakuwa na mpango wa muda mfupi wa kuwawezesha watoto wetu wanaosoma katika shule ambazo zimeathirika, zimebomoka au kuchukuliwa ni na maji, mpango wa muda mfupi ni kuhakikisha kwamba tunawawzesha vijana hawa wasirudi nyuma katika kusoma na kuwatengenezea mazingira ambayo yatawafanya waendelee na masomo, kwa hiyo wataalmu wetu watatushauri ni njia ipi ambayo itawawezesha vijana hawa kuendelea na masomo yao tukitambua kuwa wapo vijana wanaojiandaa na mitihani watakuwa nayo mwaka huu.

Mchengerwa alisema Mpango wa muda mrefu, sekta zetu zitakaa pamoja na sekta zingine ambazo zitahusika ili kuweza utaratibu wa mpango bora wa matumizi ya ardhi na kuzuia utoaji wa vibali vya ujenzi wa shule kwenye maeneo hatarishi.

“Tutawataka watalamu wetu katika ngazi ya halmashauri na mikoa kuweza kudhibiti maafa ambayo pengine tungeweza kuchukua hatua na kuyaondoa.”

Kwa upande wa Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda alisema mkakati wao ni kuhakikisha wanafunzi hao wanarudi kwenye masomo ndani ya muda mfupi.

“Wanaweza kuchelewa wiki moja au mbili lakini tutajitahidi tuwarudishe kwenye masomo haraka iwezekanavyo hasa kwa wale wanaojiandaa na mitihani ya taifa kwa mwaka huu.”

Pia Profesa Mkenda alisema kikoa hicho pia kimefanyika ikiwa ni kujadili mikakati ya utekelezaji wa sera ya elimu na mafunzo ya Ufundi ya mwaka 2024 Toleo ya 2023 kama Rais Samia Suluhu Hassan alivyoagizwa.

“ Pia kuna suala la miundombinu na rasilimali watu kwa ajili ya kazi hii, nafurahi kusema tuliyokubaliana hapa ni makubwa sana, tunamwelekeo mzuri na tunamategemeo makubwa kwamba rasilimali tulizoziziweka mpaka mwaka 2025/26 tutazitumia mapema zaidi.”

Post a Comment

0 Comments