MAADHIMISHO ya Sherehe za Mei Mosi Kitaifa kwa Mwaka 2024 yanatarajiwa kufanyika Jijini Arusha katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid na Mgeni Rasmi atakuwa Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Aprili 17, 2024 Jijini Arusha, Rais wa TUCTA, Tumaini Nyamhokya amesema maadhimisho hayo yataenda sambamba na michezo mbalimbali ya Mei mosi itakayofunguliwa rasmi siku ya Jumamosi tarehe 20 Aprili 2024 na Wazri wa Kazi, Vijana Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe. Deogratious Ndejembi.
Amesema Maadhimisho hayo yameratibiwa na Vyama vyote 13 vinavyounda Shirikisho la vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) ambavyo ni; - CHODAWU, COTWU (T), CWT, DOWUTA, RAAWU, TALGWU, TAMICO, TASU, TEWUTA, TRAWU, TPAWU, TUGHE na TUICO.
"TUCTA imeshirikiana na vyama vyote vilivyo nje ya TUCTA vilivyojitokeza katika maandalizi haya ya Sherehe za Mei Mosi ambayo yatakuwa ya aina yake". Amesema
Pamoja na hayo amewahimiza Wafanyakazi wote waliopo Mkoa wa Arusha na Mikoa ya Jirani kujumika kwa pamoja siku ya kilele cha maadhimisho ya Mei mosi Kitaifa ili kusherekea kwa pamoja na kuienzi siku hiyo muhimu kwa wafanyakazi Duniani.
0 Comments