Ticker

6/recent/ticker-posts

ORYX GAS YAGAWA BURE MAJIKO YA GESI KWA WAHARIRI, WAANDISHI DAR

Na Mwandishi Wetu
          
KAMPUNI ya Oryx Gesi Tanzania imegawa mitungi ya gesi 100 ya kilo 15 yakiwa na majiko yake yenye sahani mbili kwa wahariri na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali ikiwa ni sehemu ya mpango wake wa kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia nchini.

Akizungumza leo Aprili 30,2024 wakati wa hafla fupi ya ugawaji wa mitungi hiyo  iliyofanyika Kigamboni Dar es salaam Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni hiyo Benoit Araman amesema lengo la kugawa mitungi kwa waandishi ni muendelezo wa kuunga mkono juhudi za za Rais Dk Samia Suluhu Hassan ambaye amedhamiria kuona matumizi ya nishati safi yanapewa kipaumbele.

Ameeleza kuwa Oryx imekuwa na kampeni maalum ya kuhakikisha inaiwezesha jamii kutumia nishati safi,hivyo imekuwa ikigawa mitungi bure kwa makundi mbalimbali katika jamii na leo wamewafikia Wahariri na waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari.

"Tunafahamu kuwa waandishi wa habari  wanamchango mkubwa wa kuleta mabadiliko chanya, wanafanya kazi kubwa ya kuuhabarisha umma Hivyo kwa kutambua mchango wao hivyo Oryx tumeona ni busara pia kugawa mitungi kwa wadau hawa muhimu ambao wahariri na waandishi wa habari.

"Oryx Gas tukio hili tumelipa uzito mkubwa na hii inatokana na umuhimu wenu katika jamii yetu.Kwetu  vyombo vya habari vimekuwa daraja na kiunganishi kikubwa cha kufikisha taarifa zinazohusiana na nishati safi ya kupikia na hasa inayotokana na gesi ya oryx kwa jamii,"amesema Araman.

Amefafanua Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ameeleza dhamira yake kubwa  ni kuona ifikapo mwaka 2032 asilimia 80 ya Watanzania iwe inatumia nishati safi ya kupikia, Oryx Gas wamedhamiria kwa vitendo kufanikisha ndoto ya Rais 

"Tumekuwa tukigawa mitungi ya gesi na majiko yake bure kwa makundi mbalimbali yakiwemo ya baba na Mama Lishe,watumishi wa sekta ya afya na wajasiriamali.Tunayofuraha leo kukutana nanyi wahariri na waandishi wa habari katika tukio hilo la kuwakabidhi mtungi wa gesi wenye kilo 15 ukiwa na plate zake mbili

Aidha amesema kama ambavyo wamekuwa wakiahidi siku zote wataendelea na kampeni hiyo kadri ya uwezo wao lengo ni kuona wanafikiwa wananchi wengi zaidi 

"Oryx Ges Tanzania mpaka sasa tumeshatoa mitungi ya gesi zaidi ya 33,000 maeneo mbalimbali nchini na kiasi cha Sh  bilioni 1.5 kimeshatumika,"amesema na kuongeza wanakabidhi mitungi hiyo kwa Wahariri na waandishi wakiamini  ni kundi lenye ushawishi mkubwa hivyo watahamasisha na kuwa mabalozi kwa jamii.
MKURUGENZI Mkuu wa Kampuni ya Orxy Energies, Benoit Araman, akikabidhi jiko na mtungi wa gesi kwa Mkurugenzi wa D M News, David John, katika hafla kukabidhi vifaa hivyo kwa wahariri na waandishi wa habari, Kigamboni, Dar es Salaam, jana.
MKURUGENZI Mkuu wa Kampuni ya Orxy Energies, Benoit Araman, akikabidhi jiko na mtungi wa gesi kwa mwandishi wa habari wa Michuzi Media, Chalila Kibuda, katika hafla kukabidhi vifaa hivyo kwa wahariri na waandishi wa habari, Kigamboni, Dar es Salaam, jana.
MKURUGENZI Mkuu wa Kampuni ya Orxy Energies, Benoit Araman, akizungumza na wahariri na waandishi wa habari, kabla ya kukabidhi majiko na mitungi wa gesi ya kupikia, Kigamboni, Dar es Salaam, jana.
Meneja wa Masoko wa Oryx Energies Peter Ndomba akitoa elimu juu ya namna bora ya kutumia gesi safi ya kupikia ya Oryx. Leo jijini Dar es Salaam.
MKURUGENZI Mkuu wa Kampuni ya Orxy Energies, Benoit Araman, akikabidhi Mpigapicha Mwandamizi, Suleiman Mpochi, jiko na mtungi wa gesi ya kupikia katika hafla ya kukabidhi vifaa hivyo kwa wahariri na waandishi wa habari, Kigamboni, Dar es Salaam, jana.
Wahariri na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali wakiwa kwenye hafla ya kukabidhiwa mitungi 100 ya kupikia ya Oryx gas ya kilo 15 Kigamboni, Dar es Salaam, jana.
 

Sehemu ya mitungi ya gesi na majiko yaliyotolewa kwa wahariri na waandishi wa habari kutoka Oryx Energies Tanzania.

MKURUGENZI Mkuu wa Kampuni ya Orxy Energies, Benoit Araman, akiwa na wahariri na waandishi wa habari, baada ya kukabidhi majiko na mitungi ya gesi ya kupikia, Kigamboni, Dar es Salaam, jana.

Post a Comment

0 Comments