NA EMMANUEL MBATILO
KLABU ya Simba imeondolewa na timu ya Mashujaa Fc kwa mikwaju ya penati kwenye michuano ya CRDB Bank Federation Cup katika hatua ya 16 bora.
Katika mchezo huo ambao ulipigiwa kwenye dimba la Lake Tanganyika mkoani Kigoma, Mashujaa Fc walianza kupata bao kupitia kwa mshambuliaji wao hatari Reliant Lusajo dakika ya 5 ya mchezo na kuwapeleka hadi mapumziko wakiwa mbele kwa bao 1-0.
Mpaka mapumziko Mashujaa Fc walipata kadi nyekundu kupitia kwa kiungo wao mkabaji Said Makapu na kuwafanya kucheza nusu kwa kipindi cha pili na kuwafanya Simba Sc kupata bao la kusawazisha kupitia kwa mshambuliaji wao Freddy Michael.
Hadi dakika 90 ya mchezo mechi ilimalizika kwa 1-1 na kufanya waende kwenye mikwaju ya penati 6-5.
0 Comments