Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kwa kipindi cha miaka mitatu, jumla ya leseni za ubora wa bidhaa 2,106 zilitolewa kwa wazalishaji mbalimbali wa bidhaa hapa nchini sawa na asilimia 105.3 ya lengo la kutoa leseni 2,000.
Hayo yameelezwa leo Aprili 15, 2024 na Mkurugenzi Mkuu-TBS, Dkt. Athuman Ngenya wakati akizungumza na wahariri na waandishi wa Habari katika mkutano ulioandaliwa na ofisi ya Msajili wa Hazina
Pia katika Kuhakikisha soko linakuwa na bidhaa zenye ubora, TBS imeendelea kufanya ukaguzi wa bidhaa zinazotoka nje ya nchi kwa kutumia mfumo wa Pre- Shipment Verif cation of Conformity to Standards (PVOC) pamoja na kufanya ukaguzi pindi bidhaa zinapowasili nchini.
Dkt. Ngenya alisema kwa kipindi cha miaka mitatu, jumla ya shehena 100,851 kabla hazijaingizwa nchini sawa na asilimia 99 ya lengo la kukagua shehena 102,083. Pia, jumla ya bidhaa 151,570 kutoka nje ya nchi zilikaguliwa baada ya kuf ka nchini sawa na asilimia 77 ya lengo la kukagua bidhaa 197,417.
"TBS hudhibiti ubora wa bidhaa zinazoingizwa nchini kutoka nje kwa kutumia mfumo wa Pre- Shipment Verif cation of Conformity to Standards (PVOC) pamoja na kufanya ukaguzi pindi bidhaa zinapowasili nchini (Destination Inspection)."
Kuhusu Usajili wa bidhaa za chakula na vipodozi Dkt. Ngenya alisema
Kwa kipindi cha miaka mitatu, jumla ya shehena 100,851 kabla hazijaingizwa nchini sawa na asilimia 99 ya lengo la kukagua shehena 102,083.
Pia, jumla ya bidhaa 151,570 kutoka nje ya nchi zilikaguliwa baada ya kuf ka nchini sawa na asilimia 77 ya lengo la kukagua bidhaa 197,417.
Aidha Dkt. Nyenya alisema wamefanikiwa kufanya kaguzi mbalimbali za kushtukiza katika masoko ya ndani ambapo kaguzi hizo huzifanya mara kwa mara sokoni na viwandani kwa ajili ya kuhakikisha bidhaa zilizopo zinakidhi matakwa ya viwango husika.
Alisema TBS pia hushirikiana na taasisi nyingine za Serikali kama TRA, FCC, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Jeshi la Polisi pamoja na vyombo vingine vya usalama kufanya ukaguzi ili kubaini bidhaa zisizokidhi matakwa ya viwango na kuchukua hatua stahiki.
Kuhusu kutoa elimu kwa Umma na Wadau juu ya masuala ya viwango Dkt. Ngenya amesema TBS hutoa elimu kwa umma kupitia njia mbalimbali ili kukuza uelewa juu ya masuala ya viwango na udhibiti ubora
"Tunashiriki katika makongamano, maonesho, warsha na semina, tunaandaa mikutano na wadau wa masuala ya viwango (Stakeholder's meeting), tunaendesha kampeni za elimu kwa umma katika ngazi za wilaya na mashuleni, tunatoa elimu kutumia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii, tunaandaa matangazo, majarida na vipeperushi na tunatoa mafunzo mbalimbali kuhusu masuala ya ubora na usalama."
Kadhalika, TBS wamefanikiwa kusogeza huduma karibu na wananchi ikiwemo kujenga Maabara katika Mikoa ya kimkakati
"Shirika linatekeleza mradi wa ujenzi wa Makao Makuu ya Shirika na maabara (Viwango House Dodoma). Maabara hii itahudumia mikoa mitatu (3) ya kanda ya Kati ambayo ni Dodoma, Singida na Tabora pamoja na mikoa mingine ya karibu." Alisema Dkt. Ngenya.
0 Comments