Ticker

6/recent/ticker-posts

HATUWEZI KUIKOSOA SERIKALI KAMA SISI WENYEWE HATUWEZI KUTIMIZA WAJIBU WETU - DKT. NCHIMBI

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Ndugu. Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi amewataka Viongozi mbalimbali wa Chama Cha Mapinduzi CCM kwa ngazi zote kutimiza wajibu wao ipasavyo.
Ameyasema hayo kwenye Mkutano wa kueleza muelekeo wa Chama pamoja na mambo mengine kuhusu uelekeo wa uchaguzi wa serikali za mitaa wa mwaka huu wa 2024 na uchaguzi mkuu wa mwaka 2024.

Aidha amesema kuwa CCM inajumla ya mashina 246,000 na kila shina lina viongozi 5 ambapo inapelekea kuwa na zaidi ya viongozi Milioni moja katika ngazi hiyo na kutokana na uwepo wa viongozi wao.

Amesema kwa kuambatana na viongozi wengine wa sekretarieti ya CCM Taifa wamefika ili kuona ufanisi wa kazi kwa viongozi kuanzia Mashina hadi Mkoa kwakuwa uwepo wa ufanisi mzuri wa kazi zao ndio unaweza kuwafanya kuweza kuikosoa serikali na kutoa ushauri na muongozo kwa maslahi mapana ya Watanzania.

" Hatuwezi kuikosoa serikali tunayoiongoza kama sisi wenyewe hatuwezi kutimiza wajibu wetu. Ndio maana tumeanza kujikagua wenyewe kisha tuwe na ujasiri wa kuikosoa serikali, sasa nawapongeza shina namba tana la paraides pale majengo, mnaifanya kazi yenu vizuri sana. "Alisema Dkt. Nchimbi

Mkutano huu umekutanisha, Wajumbe wa Mashina na Wenyeviti wa Mitaa, Vijiji na Vitongoji na Miitaa, Viongozi wa Chama ngazi zote, Wazee mashuhuri, Viongozi wa Dini pamoja na Watendaji wa serikali ngazi zote na Taasisi zisizo za kiserikali.

Post a Comment

0 Comments