Na: Mwandishi Wetu - Kilimanjaro
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Zanzibar, Mhe. Fatma Rajab amewahimiza wakazi wa kilimanjaro pamoja na maeneo ya karibu kushiriki kikamilifu katika uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru, Mkoani Kilimanjaro.
Aidha, uzinduzi huo utafanyika Aprili 2, 2024 katika uwanja wa michezo wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MoCU).
Mhe. Fatma ameyasema hayo wakati wa mbio fupi maarufu (Jogging) leo Machi 30,2024 .
Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Nurdin Babu amesema kuwa Mwenge umerudi nyumbani hivyo ni vyema wanachi wakajitokeza kwa wingi.
Mbio hizo fupi ziliandaliwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ikiwa ni sehemu ya Uhamasishaji wa Uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Mkoani humo.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Maendeleo ya Jamii, Mhe. Fatma Rajab (wa tatu kutoka kulia) akiwa katika mazoezi ya kukimbia mbio fupi maarufu (jogging) ikiwa sehemu ya kuhamasisha wakazi wa kilimanjaro kushiriki katika uzinduzi wa mbio za Mwenge wa Uhuru. Wa nne kutoka kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mhe. Nurdin Babu na Katibu Tawala wa Mkoa huo, Tixon Nzunda.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mhe. Nurdin Babu akizungumza na wakazi wa mkoa huo kuhusu shughuli ya uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru katika mkoa huo.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Zanzibar, Mhe. Fatma Rajab akihamasisha wakazi wa Kilimanjaro kujitokeza katika uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru zutakazofanyika katika mkoa huo.
0 Comments