Ticker

6/recent/ticker-posts

STEVE NYERERE AWAVAA WANAOMBEZA RAIS SAMIA MITANDAONI

Mwenyekiti wa Taasisi ya Mama Ongea na Mwanao Steve Nyerera akizungumza na waandishi wa habari leo Machi 11, 2024 Jijini Dar es Salaam.

*****************

TAASISI ya Mama Ongea na Mwanao imelitaka Jeshi la Polisi kuwakamata na kuwahoji watu wote wanaomtukana Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Hayo yamebainishwa leo Machi 11, 2024 na Mwenyekiti wa Taasisi hiyo Steve Nyerera akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

Kauli hiyo inakuja baadaa ya siku chache kijana Mmoja kumbeza Rais Dkt. Samia kwenye mitandao ya kijamii akimwita kuwa ni mama wa Vikoba.

Hivyo Nyerere amewataka watu wote wanaosema wapo karibu na Rais Dkt. Samia kuhakikisha wanapambana na wanaomtukana.

Katika hatua nyingine Taasisi hiyo imesema hivi karibini wanatarajiwa kufanya tamasha kubwa la walemavu Nchi nzima na kuwapatia mahitaji yao mbalimbali ya msingi.

Amesema Taasisi ya Mama ongea na mwanao ipo tayari kuunga juhudi za Rais Dkt Samia Suluhu Hassan katika kuwasaidia makundi maalumu kwenye jamii.

"Sisi kama Taasisi tunawaahidi tutaendelea kuwashika mkondo nyinyi ni wapiga kura nchi hii, nyinyi ni watu kama watu wengine na mnahaki sawa na wengine".

Pia Steve amesema Mama Samia amekuwa akijikita katika kusaidia Watanzania wa hali ya chini,katika kipindi cha miaka mitatu yake ya uongozi tunampongeza.

"Mama ameona tatizo la umeme na kulitaftia ufumbuzi na kujenga bwawa la mwalimu nyerere ambalo likianza kutoa huduma tutauza umeme mpaka nje ya Tanzania".

Post a Comment

0 Comments