Ticker

6/recent/ticker-posts

RAIS SAMIA AWATAKA WATANZANIA KUYAISHI MAISHA YA HAYATI MWINYI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan  akizungumza wakati wa kuaga Mwili wa Rais Mstaafu wa awamu ya pili Hayati Mzee Ali Hassan Mwinyi katika uwanja wa Michezo wa Amani mjini Zanzibar tarehe 02 Machi 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan  na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi wakiomba Dua wakati wakitoa Heshima za mwisho kwenye Jeneza lenye Mwili wa Rais Mstaafu wa awamu ya pili Hayati Mzee Ali Hassan Mwinyi katika uwanja wa Michezo wa Amani mjini Zanzibar tarehe 02 Machi 2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Makamu wa Rais wa Namibia Mhe. Netumbo Nandi - Ndaitwah alipowasili katika uwanja wa Michezo wa Amani mjini Zanzibar kwa ajili ya kuongoza Viongozi na Wananchi wa Zanzibar kutoa Heshima za mwisho kwa Rais Mstaafu wa awamu ya pili Hayati Mzee Ali Hassan Mwinyi aliyefariki dunia tarehe 29 Februari 2024 katika Hospitali ya Mzena Jijini Dar es salaam alipokuwa akipata matibabu ya Saratani ya Mapafu, ambapo anatarajiwa kuzikwa Kijijini kwake Mangapwani Mkoa wa Kaskazini Unguja tarehe 02 Machi 2024.
Viongozi Wastaafu mbalimbali wakiwa katika uwanja wa Michezo wa Amani mjini Zanzibar kwa ajili ya kutoa Heshima za mwisho kwa Rais Mstaafu wa awamu ya pili Hayati Mzee Ali Hassan Mwinyi aliyefariki dunia tarehe 29 Februari 2024 katika Hospitali ya Mzena Jijini Dar es salaam alipokuwa amelazwa akipata matibabu ya  Saratani ya Mapafu, ambapo anatarajiwa kuzikwa Kijijini kwake Mangapwani Mkoa wa Kaskazini Unguja tarehe 02 Machi 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza jambo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi wakati wa Hafla ya kutoa Heshima za mwisho kwa Rais Mstaafu wa awamu ya pili Hayati Mzee Ali Hassan Mwinyi katika uwanja wa Michezo wa Amani mjini Zanzibar. Hayati Mzee Mwinyi alifariki dunia tarehe 29 Februari 2024 katika Hospitali ya Mzena Jijini Dar es salaam alipokuwa amelazwa akipata matibabu ya Saratani ya Mapafu, na anatarajiwa kuzikwa Kijijini kwake Mangapwani Mkoa wa Kaskazini Unguja tarehe 02 Machi 2024.
Wajane wa Hayati Rais Mstaafu awamu ya pili Mzee Ali Hassan Mwinyi Bibi Siti Mwinyi na Khadija Mwinyi wakiwasili katika Uwanja wa Michezo wa Amani mjini Zanzibar  tarehe 02 Machi 2024.
Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ waliobeba Jeneza lenye Mwili wa  Rais Mstaafu awamu ya pili Mzee Ali Hassan Mwinyi wakiwasili katika Uwanja wa Michezo wa Amani mjini Zanzibar  tarehe 02 Machi 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa pamoja na Viongozi mbalimbali katika uwanja wa Michezo wa Amani mjini Zanzibar kwa ajili ya kuongoza Viongozi na Wananchi wa Zanzibar kutoa Heshima za mwisho kwa Rais Mstaafu wa awamu ya pili Hayati Mzee Ali Hassan Mwinyi aliyefariki dunia tarehe 29 Februari 2024 katika Hospitali ya Mzena Jijini Dar es salaam alipokuwa amelazwa akipata matibabu ya  Saratani ya Mapafu, ambapo anatarajiwa kuzikwa Kijijini kwake Mangapwani Mkoa wa Kaskazini Unguja tarehe 02 Machi 2024.
Makamu wa Rais wa Namibia Mhe. Netumbo Nandi  Ndaitwah akizungumza na waombolezaji wakati wa kuaga Mwili wa Rais Mstaafu wa awamu ya pili Hayati Mzee Ali Hassan Mwinyi katika uwanja wa Michezo wa Amani mjini Zanzibar tarehe 02 Machi 2024.
Famili ya Hayati Mzee Ali Hassan Mwinyi ikiwa katika uwanja wa Michezo wa Amani mjini Zanzibar kwa ajili ya kutoa Heshima za mwisho kwa Rais Mstaafu wa awamu ya pili Hayati Mzee Ali Hassan Mwinyi aliyefariki dunia tarehe 29 Februari 2024 katika Hospitali ya Mzena Jijini Dar es salaam alipokuwa amelazwa akipata matibabu ya  Saratani ya Mapafu, ambapo anatarajiwa kuzikwa Kijijini kwake Mangapwani Mkoa wa Kaskazini Unguja tarehe 02 Machi 2024.
Wananchi waliohudhurua katika uwanja wa Michezo wa Amani mjini Zanzibar kwa ajili ya kutoa Heshima za mwisho kwa Rais Mstaafu wa awamu ya pili Hayati Mzee Ali Hassan Mwinyi aliyefariki dunia tarehe 29 Februari 2024 katika Hospitali ya Mzena Jijini Dar es salaam alipokuwa amelazwa akipata matibabu ya Saratani ya Mapafu, ambapo anatarajiwa kuzikwa Kijijini kwake Mangapwani Mkoa wa Kaskazini Unguja tarehe 02 Machi 2024.

Post a Comment

0 Comments