Ticker

6/recent/ticker-posts

RAIS DKT. MWINYI AJUMUIKA NA WAUMINI WA DINI YA KIISLAMU KATIKA DUA YA KUMUOMBEA HAYATI MZEE ALI HASSAN MWINYI

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi amejumuika na waumini wa dini ya Kiislamu na waombolezaji katika Dua ya khitma ya kumuombea aliyekuwa Rais wa Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Marehemu Mzee Ali Hassan Mwinyi ambayo inafanyika leo tarehe: 03 Machi 2024, katika viwanja vya maonesho Nyamanzi, Mkoa wa Mjini Magharibi, Unguja.

Dua hiyo imeandaliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kumuombea Marehemu Mzee Mwinyi ambaye amefariki dunia tarehe: 29 Februari 2024 katika hospitali ya Mzena, Dar es Salaam na kuzikwa tarehe: 02 Machi 2024 Mangapwani, Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Aidha, dua hiyo umehudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Serikali, Chama, Dini na wananchi.

Post a Comment

0 Comments