Mtendaji Mkuu wa OSHA, Bi Khadija Mwenda (watatu
kulia) akiambatana na baadhi ya viongozi wa OSHA katika ziara yake ya
kutembelea mradi wa kufua umeme wa Julius Nyerere (JNHPP) kwa lengo la
kufuatilia zoezi la tathmini ya vihatarishi vya usalama na afya katika mradi
huo iliyofanywa na wataalamu wa OSHA
hivi karibuni.
Mtendaji Mkuu wa OSHA, Bi Khadija Mwenda
akisisitiza jambo kwa Kaimu Meneja wa Mradi wa kufua umeme wa Julius Nyerere
(JNHPP), Mhandisi. Mathew Bundala wakati wa ziara yake katika mradi huo
akiambatana na baadhi ya viongozi wa OSHA kwa lengo la kufuatilia zoezi la
tathmini ya vihatarishi vya usalama na afya katika mradi huo.
Mtendaji Mkuu wa OSHA, Bi Khadija Mwenda
(katikati) Pamoja na baadhi ya viongozi wa OSHA wakipokea maelezo kutoka kwa Kaimu
Meneja wa Mradi wa kufua umeme wa Julius Nyerere (JNHPP), Mhandisi. Mathew
Bundala wakati wa ziara iliyolenga kufuatilia zoezi la tathmini ya vihatarishi
vya usalama na afya katika mradi huo iliyofanywa na wataalamu wa OSHA hivi
karibuni
Mtendaji Mkuu wa OSHA, Bi Khadija Mwenda akisisitiza
juu ya umuhimu wa kufanya tathmini ya vihatarishi vya usalama na afya katika
maeneo ya kazi wakati wa ziara yake ya kutembelea mradi wa kufua umeme wa
Julius Nyerere (JNHPP).
Mtendaji Mkuu wa OSHA, Bi Khadija Mwenda pamoja na baadhi ya viongozi na watumishi wa OSHA wakifuatilia muhtasari wa mradi wa kufua umeme wa Mwalimu Julius Nyerere (JNHPP) na namna ambavyo mradi huo utamaliza kero ya umeme nchini pindi utakapokamilika uliowasilishwa na Mhandisi Dismas Mbote (mbele).
0 Comments