Ticker

6/recent/ticker-posts

ORYX GAS WAMKOSHA MAKAMU WA RAIS, ATOA MWITO KWA TAASISI BINAFSI

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

MAKAMU wa Rais Dk.Philip Mpango ametoa mwito kwa sekta binafsi kuunga mkono na kuchangia katika kampeni ya kuondokana na matumizi ya nishati chafu huku akiipongeza kampuni ya Oryx Gas kwa namna inavyoriki kwa vitendo kuhamasisha matumizi ya nishati hiyo kwa kugawa mitungi ya gesi.

Dk.Mpango ameyasema hayo alipokuwa akifungua Kongamano la Wanawake la kugawa mitaji na vitendea kazi vya nishati safi ya kupikia yakiwemo majiko ya gesi ya Oryx.

Wakati anazungumza kuhusu nishati safi katika Kongamano hilo Dk.Mpango ameeleza baadhi ya sekta binafsi zinaweza kusaidia kuwekeza katika utafiti, ubunifu na uzalishaji wa nishati safi na nafuu ya kupikia.

“Naiomba sekta sekta binafsi kutumia mifuko ya wajibu wenu kwa jamii kuwezesha kaya zinazowazunguka kupata nishati safi ya kupikia mijini na vijijini.

“Sekta binafsi pia inaweza kushirikiana na watu binafsi kueneza matumizi ya nishati safi ya kupikia.Kwa mfano kampuni ya Oryx Gas inafanya kazi na taasisi ya Dorris Mollel Foundation kusaidia akina mama katika maeneo mbalimbali ya nchi yetu.”

Aidha Dk.Mpango ametoa rai kwa Oryx pamoja na wadau wengine kuendelea kuongeza nguvu katika kuunga mkono kampeni ya nishati safi ya kupikia nchini.

Awali akizungumza katika kongamano hilo Mkurugenzi wa Oryx Gas Tanzania Benoit Araman amesema imeweka mkakati maalum katika kukuza matumizi ya nishati safi ya kupikia ambapo mpaka sasa wameshatoa mitungi ya gesi na majiko yake zaidi ya 24000 yenye thamani ya Sh.bilioni 2 kwa makundi mbalimbali ya wanawake.

“Kwa zaidi ya miaka 15, upatikanaji wa suluhisho la kupikia kwa nishati safi umekuwa ukijadiliwa na kupangwa, lakini sasa imekuwa mada ya muhimu, chini ya uongozi wa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan na serikali yake.

Amesema kuwa takwimu zinaonesha nchini Tanzania, wananchi 33,000 wanapoteza maisha kila mwaka kwa kuvuta moshi na chembechembe zinazotokana na mkaa na kuni, hivyo kupika kwa gesi ya Oryx itatatua changamoto hiyo.

Pia amesema kupika kwa gesi kunasaidia katika kulinda mazingira kwani huzuia ukataji miti, hivyo husaidia kulinda mazingira

Kuhusu hali za maisha amesema kupika kwa kutumia gesi ya Oryx huzuia wanawake kutumia saa nyingi kwa ajili ya kukusanya kuni kutoka msituni huku pia akielezea namna ambavyo gesi inavyosaidia wanawake kukabiliwa na hatari katika misitu ya wanyamapori pamoja na kukutana na majanga mengine.

“Kupika kwa kutumia gesi ya Oryx ni kupika kwa haraka na kwa ufanisi kwa hivyo kutawaruhusu wanawake kuwa na muda zaidi kusoma, kufanya kazi za jamii na maendeleo ya kibinafsi.

“Kupika kwa kutumia gesi ya Oryx ni kupika kwa haraka na kwa ufanisi zaidi; kwa hiyo, wanawake wataanda chakula kwa wakati na wanaume hawatalalamika juu ya kuchelewa kwa chakula kinachosababisha mizogo.

“Timu nzima ya Oryx Gas Tanzania inajivunia kufanya kazi kila siku kusaidia mpango wa upatikanaji wa upishi kwa nishati safi kwa wakazi wa Tanzania. Kwa hivyo, Oryx Gas itaendelea kufanya kazi kwa bidii ili kutekeleza maono ya Rais kuhusu upatikanaji wa nishati safi,”amesema Benoit.

Pia amesema anaishukuru Serikali kwa kuwaunga mkono katika mipango yao ya nishati safi kwa kuhakikisha matumizi ya gesi ya Oryx jijini Dodoma na Tanzania kwa ujumla.
Makamu wa Rais Dk Philip Mpango (kushoto) akimsikiliza  Mkurugenzi wa Oryx Gas Tanzania ,Benoit Araman wakati alipotembelea banda la kampını hiyo kwenye kongamano la wanawake la kugawa  mitajdi na vitendeakazi vya nishati ya kupikia lililofanyika Jijini Dodoma
Meneja Masoko wa Kampuni ya Oryx Gas Peter Ndomba( kushoto) akitoa elimu ya matumizi sahihi ya kutumia jiko la gesi la Oryx kwa Makamu wa Rais Dk.Philip Mpango  baada ya kutembelea Banda la Kampuni hiyo wakati wa Kongamano la Nishati Safi lililofanyika Dodoma .Katikati ni Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dk .Dotto Biteko akisikiliza kwa makini maelezo hayo
Mkurugenzi wa Kampuni ya Oryx Gas Araman Benoit akizungumza wakati wa Kongamano la Nishati Safi lililofanyika Dodoma na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Makamu wa Rais DK Philip Mpango aliyekuwa mgeni rasmi .Katika maelezo yake Benoit ameeleza hadi sasa Kampuni hiyo imeshagawa mitungi ya gesi 24000 yenye thamani ya Sh.bilioni 2.alikuwa akiongea kuhusu minajati mbalimbali ambapo Otyx imejiwekea ktk kukuza matumizi ya nishati safi ya kupikia ambapo hadi sssa tumeshatoa majiko zaidi ya 24000 yenye thamani ya zaidi ya bilion 2 kwa makundi mbalimbali ya wanawake nchini

Post a Comment

0 Comments