Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhandisi Cyprian Luhemeja amekagua maandalizi ya shughuli za uzinduzi mbio za Mwenge wa Uhuru zitakazofanyika Aprili 2, 2024 Mkoani Kilimanjaro.
Akiwa katika ukaguzi huo leo Machi 30, 2024 Mhandisi Luhemeja aliambatana na Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Fatma Rajab na Katibu Tawala wa Mkoa huo, Tixon Nzunda ambapo wamekagua uwanja wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi, vijana wa halaiki na vikundi vya burudani.
Mwenge wa Uhuru utakimbizwa katika mikoa 31 na Halmashauri 195 ambapo kwa mwaka huu 2024 zinaongozwa na kauli mbiu isemayo " Tunza Mazingira na Shiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa Ujenzi wa Taifa Endelevu".
Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhandisi Cyprian Luhemeja akizungumza na Waratibu wa Mwenge wa Uhuru wa Mikoa wakati wa ziara yake iliyolenga kukagua maandalizi ya uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru zitakazofanyika katika uwanja wa michezo wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MoCU), Aprili 2, 2024 Mkoani Kilimanjaro.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhandisi Cyprian Luhemeja akizungumza na kijana wa halaiki Prince Kamiliminde wakati akikagua maendeleo ya maandalizi ya uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru zitakazofanyika Aprili 2, 2024 katika uwanja wa michezo wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MoCU), Mkoani Kilimanjaro.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhandisi Cyprian Luhemeja akiangalia sehemu ya mazoezi ya vijana wa halaiki wakati akikagua maendeleo ya maandalizi ya uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru zitakazofanyika Aprili 2, 2024 katika uwanja wa michezo wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MoCU), Mkoani Kilimanjaro.
0 Comments