Na: Mwandishi wetu, DAR ES SALAAM.
Taasisi ya Foundation For Civil Society FCS, imeungana na wadau wengine wa Asasi za Kiraia na ubalozi wa Denmark kusherehekea miaka 62 ya mashirikiano kati ya Serikali ya Tanzania na Denmark.
Akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika Machi 21, 2024 Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa FCS anayemaliza muda wake Francis Kiwanga, amesema ushirikiano baina ya Mataifa hayo yamekuwa na manufaa makubwa katika kuchochea kasi ya maendeleo kwa wananchi.
Ameeleza kuwa katika kipindi cha miaka 20 ya FCS imeweza kufanya kazi kwa karibu na ubalozi wa Denmark kwa miaka 14 mfululizo kupitia Shirika lake la Maendeleo DANIDA na kuwawezesha kufanyakazi na Asasi za Kiraia zaidi ya 6000 zilizopo katika mikoa na wilaya zote za Tanzania Bara na Zanzibar.
"Katika kipindi cha miaka 14, tumepata rasilimali fedha ambazo zimetuwezesha kufanyakazi na taasisi zaidi ya 6000, katika kuboresha maisha na kuondoa umasikini hapa nchini" amesema Kiwanga. Nnnjjjj
Aidha amebainisha kuwa Denmark imekuwa ikishirikiana na Serikali ya Tanzania tangu kipindi cha Baba wa Taifa, na kwamba wameendelea kufanyakazi katika Awamu zote za uongozi na kwamba Sherehe hizo zinakwenda sambamba na maadhimisho ya miaka mitatu ya Awamu ya Sita ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.
Kwa upande wake Balozi wa Denmark nchini Tanzania Mette Norgaad Spandet, amesema Serikali ya Denmark itaendelea kudumisha ushirikiano uliopo na Tanzania katika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kwa kushirikiana na Asasi za Kiraia. Lol
Aidha ameipongeza FCS kwa kazi kubwa inayofanya kwa kuwafikia wananchi wengi katika miradi ya kijamii kwa kushirikiana na Asasi nyingine za Kiraia nchini.
0 Comments