Ticker

6/recent/ticker-posts

BENKI YA CRDB YAFUTURISHA WATEJA NA WENYE MAHITAJI MAALUM GEITA

 

Katika mwendelezo wa utamaduni wa Benki ya CRDB kuungana na Waumini wa Dini ya Kiislamu wanaoishiriki Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan imejumuika na wateja pamoja na makundi  yenye uhitaji maalum katika futari waliyoandaa.

Hafla ya Futari iliyoandaliwa na Benki ya CRDB imefanyika Ijumaa Machi 22,2024 katika ukumbi wa Otonde  mkoani Geita ambapo Mkuu wa Wilaya ya Chato, Mhe. Said Juma Mkumba alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe. Martine Shigela huku  Menejimenti ya Benki  ya CRDB iliwakilishwa na  Mkurugenzi wa Rasimali Watu Godfrey Rutasingwa. 

Benki ya CRDB pia imekabidhi vitu mbalimbali kwa vituo vya watu wenye mahitaji maalum vitakavyowasaidia kukamilisha funga yao  katika kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.

Benki ya CRDB ambayo mwaka 2021 ilianzisha dirisha la huduma za kibenki ambazo zimefuata misingi ya dini ya kiislamu maarufu kama Al Barakah Banking, imekuwa na utaratibu kila mwaka wakati wa Ramadhan kushiriki Futari na wateja wake na kutoa Sadaka ya vyakula kwa watu wenye mahitaji maalum.
Mkurugenzi wa rasilimali watu Godfrey Rutasingwa  akitoa salamu za benki ya CRDB
Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi ndugu Jumanne Wambura Wagana akitoa salamu za ufunguzi
Shekhe mkuu wa mkoa wa Geita Alhaj Shekhe Alhad Kabanju akitoa salamu na pongezi kwa CRDB.
Mkuu wa Wilaya ya Chato  Mh. Said Mkumba akitoa salamu kwa niaba ya mgeni wa heshima mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe. Martine Shigela
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita Sophia Jongo aliye mbele na akina mama wa Mkoa wa Geita wakati wa Iftar.


Post a Comment

0 Comments