Madereva wa kituo cha Africana wakipatiwa elimu ya utambuzi wa vitendo vya ukatili wa kijinsia na jinsi ya kupambana navyo.
Maeneo ya masoko wilayani Kinondoni pia wamefikiwa na elimu hiyo iliyotolewa na Dawati la Jinsia la kituo cha Kawe kwa udhamini wa Barrick.
Maeneo ya masoko wilayani Kinondoni pia wamefikiwa na elimu hiyo iliyotolewa na Dawati la Jinsia la kituo cha Kawe kwa udhamini wa Barrick.
Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la Polisi Kitengo cha Dawati la Jinsia na Watoto wilaya ya Kawe A/NSP Frank Mnojela akitoa elimu ya kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa Wanafunzi.
Polisi pia walitembelea waathirika wa madawa ya kulevya na kuwafikishia elimu hiyo.
Wavuvi nao walifikiwa na elimu hiyo
****
Wakati changamoto za kuwepo usafiri wa pikipiki maarufu kama bodaboda kuhusishwa na ongezeko la ajali za barabarani, ipo changamoto nyingine kubwa ya madereva wa bodaboda kudhalilisha watoto wadogo wanaotumia usafiri huo kingono , hali inayohatarisha maisha ya watoto kiafya na tishio la kuongezeka kwa mimba za utotoni katika miaka ijayo.Changamoto hiyo imebainika wakati wa kampeni ya kutoa elimu dhidi ya vitendo vya ukatili wa kijinsia ya siku 8 iliyoandaliwa na Dawati la kijinsia na watoto la kituo cha Polisi cha Kawe Jijini Dar es salaam katika mwendelezo kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani kwa udhamini wa kampuni ya Barrick.
Baadhi ya madereva wa bodaboda wa kituo cha Africana kilichopo wilayani Kinondoni wakiongea baada ya kupatiwa mafunzo hayo walieleza kukithiri kwa vitendo vya baadhi ya madereva wenzao kudhalilisha watoto kingono na wameeleza kuwa chanzo ni wazazi ambao wanawakabidhi watoto wawasafirishe kwenda mashuleni katika mazingira yasio rafiki.
Walieleza kuwa watoto wadogo wa kike wamekuwa wakielekezwa na wazazi wao kuwakumbatia madereva wanapokuwa wamebebwa kwenye usafiri wa pikipiki hali inayosababisha watoto kuwazoea madereva hao na wasio na maadili hutumia nafasi hiyo kuwadhalilisha watoto sambamba na kuwaingiza katika vitendo vya ngono katika umri mdogo.
Akiongea wakati wa kuhitimisha mafunzo hayo mwishoni mwa wiki , Mkuu wa Dawati hilo ASP Elizabeth Msabila, alisema mafunzo yamefanyika katika maeneo mbalimbali ya jamii na kufikia makundi mbalimbali wakiwemo wafanyabiashara wa vyakula na wauza kuku katika soko la Kawe , wauzaji wa pombe za kienyeji na watumiaji wa madawa ya kulevya (mateja) katika eneo la Rungwe Bandani Mbezi . Kawe beach kwa vijana wa Beach boys, na Wanafunzi wa shule ya Sekodari ya Mtakuja iliyopo Kunduchi Beach Mtongani.
Msabila, alisema katika utoaji wa elimu hiyo wamegundua kuwa taifa lipo kwenye hatari kubwa ya kupoteza nguvu kazi ya vijana wa kiuume amabo wengi wamejiingiza katika vitendo vya tabia za ushoga, uvutaji wa bangi na madawa ya kulevya.
Pia alisema wamebaini kuwa watoto wengi wamekuwa wakifanyiwa ukatili na kubakwa hasa na ndugu wa karibu na kuwaasa wazazi kuhakikisha wanawalinda watoto wao kwa kuwakagua mara kwa mara kwa kuwa watoto wanaofanyiwa vitendo hivyo vya ukatili wanatishiwa kuwa wakisema watauawa na watoto wao kubaki na woga wa kutoa taarifa kwa wazazi wao.
ASP Elizabeth Msabila, alisema ili uweze kumgundua mtoto aliyebakwa moja ya dalili zake anakuwa hapendi kuchangamana na wenzake pia anakuwa mnyonge hapendi kucheza na wenzake pia anatembea kwa kuchechemea.
Aliwashukuru wananchi kwa kuwa na mwitikio mkubwa kuhudhuria mafunzo hayo sambamba na kufahamu Dawati la jinsia na watoto linavyofanya kazi na aliishukuru kampuni ya Barrick kwa kufanikisha mafunzo hayo,
Kwa upande Mkaguzi wa jeshi la Polis Dawati la Jinsia na Watoto kwa kata ya Kawe -Mbweni , wake Inspekta Ambilike Kibangu alisema wametoa elimu ya jinsi madawati ya kujinsia yaliyopo chini ya Jeshi la Polisi yanayovyofanya kazi na jinsi yanavtyoshughulikia kupambana na vitendo vya ukatili kwa watoto na Wanawake
Pia walitoa elimu juu ya aina mbalimbali za ukatili wa kijinsia ambapo alibainisha kuwa kuna aina mbalimbali za ukatili ukiwemo ukatili wa kimwili kwa watoto , udhalilishaji wa mke au mme ,mashambulizi ya aibu pamoja na ubakaji na suala zima la ulawiti kwa watoto wa kiume na watoto wa kike.
Pia wametoa elimu kwa akina mama wanaopigwa na waume zao au wanaume wanaonyanyaswa na wake zao kwa kunyimwa haki zao za unyumba kwenda dawati ili wakapatiwe ushauri juu ya kukabiliana na changamoto hiyo.
Captions
1.
2.
4.
5.
6/9-
0 Comments