Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Bulyanhulu, Bi. Joyce Lwanji,akipanda mti wakati wa hafla ya kupokea miche hiyo.
Mkurugenzi wa Kakola Digital Solution, David Semwenda akipanda mto katika hafla hiyo.
Mwakilishi wa Barrick Bulyanhulu, katika hafla hiyo, Mary Lupamba,akishiriki zoezi la kupanda miti katika shule ya msingi Bulyanhulu
Mkurugenzi wa Kakola Digital Solution David Semwenda (kulia) akimkabidhi Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Bulyanhulu, Joyce Lwanji miche ya Miti kwa ajili ya kupandwa shuleni hapo.
Sehemu ya majengo ya shule ya msingi Bulyanhulu
Sehemu ya miche ya miti iliyotolewa na Barrick Bulyanhulu na Kakola Digital Solution
Picha ya pamoja kati ya wawakilishi wa mgodi wa Barrick Bulyanhulu, Mkurugenzi wa digital solution, walimu na wanafunzi wa shule ya Msingi Bulyanhulu
****
Katika kuendeleza mkakati wake wa utunzaji wa Mazingira, mgodi wa Barrick Bulyanhulu kwa kushirikiana na kampuni ya Kakola Digital Solution ambayo ni mzabuni wa mgodi huo umetoa miche ya miti 500 ya aina mbalimbali katika shule mpya ya msingi ya Bulyanhulu, iliyopo kata ya Bulyanhulu Halmashauri ya Msalala mkoani Shinyanga.
Akizungumza baada ya kukabidhi miche hiyo, Mkurugenzi wa Kakola Digital Solution, David Semwenda, amesema wameamua kushirikiana na mgodi kutoa miche hiyo ya miti ikiwa ni kurudisha shukrani kwa jamii inayozunguka mgodi lakini ikiwa wao wanufaika na mgodi kwa kuwa wazabuni lazima warudishe kidogo wanachopata ili jamii ijivunie kuwa na kampuni za wazawa walioaminiwa na wawekezaji.
“Tunaushukuru sana mgodi wa Barrick Bulyanhulu kwa kutuamini kama vijana wazawa na kukubali kufanya kazi na sisi lakini pia kulingana na mazingira ya shule hii ni mpya na haikuwa na miti yoyote hivyo tukaona tuanze na shule hii kisha tutaendelea na shule nyingine”, David alisema
Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Bi. Joyce Lwanji, ameishukuru kampuni ya Kakola Digital na Mgodi wa Barrick Bulyanhulu kwa kuwapatia miche hiyo na kuahidi kuwa wataitunza miti hiyo ili kuwapa imani na wadau wengine kuendelea kufadhili vitu mbalimbali katika shule hiyo.
Kwa Upande wake, Mwakilishi wa Barrick Bulyanhulu katika hafla hiyo, Mary Lupamba, alisema kampuni itaendelea kushirikiana na Serikali na wadau mbalimbali katika kuwaletea maendeleo wananchi wote wanaoishi karibu na mgodi huo ili wanufaike na uwekezaji wa mgodi huo.
0 Comments