Ticker

6/recent/ticker-posts

WAZIRI MKUU AAGIZA UVUNWAJI MAJI YA MVUA

*Aiagiza Wizara ya Maji ijenge miundombinu ya kuyavuna yatumike kiangazi

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameiagiza Wizara ya Maji iongeze kasi katika uwekezaji kwenye ujenzi wa miundombinu ya kuvuna maji ya mvua pamoja na kujenga mabwawa ya kukinga maji ili yatumike wakati wa kiangazi, kwenye ukame na kuzuia mafuriko.

Pia, Mheshimiwa Majaliwa amewaagiza viongozi wa Bodi za Maji wa Mabonde waongeze jitihada katika uhifadhi wa vyanzo vya maji ikiwa ni pamoja na kuweka mipaka kwenye maeneo ya vyanzo vya maji na kutangaza maeneo hayo kwenye gazeti la Serikali kama maeneo tengefu ili kuyalinda kisheria.

Waziri Mkuu ametoa maagizo hayo leo (Jumapili, Februari 11, 2024) baada ya kufungua Mkutano wa Sita wa Jukwaa la Taifa la Sekta Mtambuka kuhusu Usimamizi na Uendeshaji wa Rasilimali za Maji katika ukumbi wa Maktaba Mpya ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

“Bodi za Maji za Mabonde zitekeleze agizo la Mheshimiwa Makamu wa Rais alilolitoa wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa ya Upandaji Miti Rafiki wa Maji katika Vyanzo vya Maji nchini iliyofanyika Tarehe 16 Novemba 2022 kwa kupanda angalau miti rafiki wa maji milioni 2.5 kwa mwaka.”

Aidha Mheshimiwa Majaliwa amesema, kwa mujibu wa takwimu za Desemba, 2022, hali ya upatikanaji wa huduma ya maji ni wastani wa asilimia 88 mijini na vijijini ni wastani wa asilimia 77. Mahitaji hayo yataendelea kuongezeka kutokana na ongezeko la watu na ukuaji wa shughuli za uzalishaji mali katika sekta mbalimbali kama kilimo nishati, viwanda, utalii, madini, mifugo na uvuvi.

Pamoja na hayo amesema, uharibifu wa mazingira, mabadiliko ya tabianchi, uchafuzi na matumizi mabaya ya maji hutishia hali ya usalama wa maji kwani husababisha kupungua kwa maji katika vyanzo mbalimbali.

"Uchafuzi wa maji hufanya yasiweze kutumika na wakati mwingine kusababisha gharama kubwa ya kuyatibu ili yaweze kutumika tena". Amesema

Kwa upande wa Wakala wa Misitu Tanzania, Waziri Mkuu amewaagiza viongozi wake wadhibiti upandaji wa miti mingi ya kibiashara katika vyanzo vya maji kwa kuwa miti ikikatwa eneo litabaki kuwa jangwa, piasuala hilo litekelezwe sambamba na kusitisha kutoa vibali vya kuvuna misitu kwenye vyanzo vya maji.

Awali, Waziri wa Maji Jumaa Aweso ametumia fursa hiyo kumshukuru na kumpongeza Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha nyingi katika ujenzi wa miradi wa maji, ambapo amesema ulindaji wa rasilimali za maji utaendelea kupewa kipaumbele nchini.

Kwa upande wake, Waziri wa Madini Anthony Mavunde ambaye ameongea kwa niaba ya mawaziri wa kisekta amesema wataendelea kushirikiana kuhakikisha kwa pamoja wanazilinda rasilimali za maji.
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akifungua Mkutano wa Sita wa Jukwaa la Taifa la Sekta Mtambuka kuhusu Usimamizi na Uendeshaji wa Rasilimali za Maji uliofanyika leo Februari 11,2024 katika ukumbi wa Maktaba Mpya ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira Mhe. Jackson Gedion Kiswaga akizungumza katika Mkutano wa Sita wa Jukwaa la Taifa la Sekta Mtambuka kuhusu Usimamizi na Uendeshaji wa Rasilimali za Maji uliofanyika leo Februari 11,2024 katika ukumbi wa Maktaba Mpya ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya Maji ya Taifa na Mwenyekiti wa Jukwaa la Kitaifa la Wadau wa Sekta Mtambuka Mhandisi Mbogo Futakamba, akizungumza katika Mkutano wa Sita wa Jukwaa la Taifa la Sekta Mtambuka kuhusu Usimamizi na Uendeshaji wa Rasilimali za Maji uliofanyika leo Februari 11,2024 katika ukumbi wa Maktaba Mpya ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso akizungumza katika Mkutano wa Sita wa Jukwaa la Taifa la Sekta Mtambuka kuhusu Usimamizi na Uendeshaji wa Rasilimali za Maji uliofanyika leo Februari 11,2024 katika ukumbi wa Maktaba Mpya ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde akizungumza katika Mkutano wa Sita wa Jukwaa la Taifa la Sekta Mtambuka kuhusu Usimamizi na Uendeshaji wa Rasilimali za Maji uliofanyika leo Februari 11,2024 katika ukumbi wa Maktaba Mpya ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Mhandisi Mwajuma Waziri akizungumza katika Mkutano wa Sita wa Jukwaa la Taifa la Sekta Mtambuka kuhusu Usimamizi na Uendeshaji wa Rasilimali za Maji uliofanyika leo Februari 11,2024 katika ukumbi wa Maktaba Mpya ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Albert Chalamila akizungumza katika Mkutano wa Sita wa Jukwaa la Taifa la Sekta Mtambuka kuhusu Usimamizi na Uendeshaji wa Rasilimali za Maji uliofanyika leo Februari 11,2024 katika ukumbi wa Maktaba Mpya ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Baadhi ya Wakuu wa Wilaya na viongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam wakiwa katika Mkutano wa Sita wa Jukwaa la Taifa la Sekta Mtambuka kuhusu Usimamizi na Uendeshaji wa Rasilimali za Maji uliofanyika leo Februari 11,2024 katika ukumbi wa Maktaba Mpya ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Baadhi ya viongozi na wadau mbalimbali wa maji wakiwa katika Mkutano wa Sita wa Jukwaa la Taifa la Sekta Mtambuka kuhusu Usimamizi na Uendeshaji wa Rasilimali za Maji uliofanyika leo Februari 11,2024 katika ukumbi wa Maktaba Mpya ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Msanii wa nyimbo na mashairi Bw. Mrisho Mpoto akitoa burudani katika Mkutano wa Sita wa Jukwaa la Taifa la Sekta Mtambuka kuhusu Usimamizi na Uendeshaji wa Rasilimali za Maji uliofanyika leo Februari 11,2024 katika ukumbi wa Maktaba Mpya ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

Post a Comment

0 Comments