Ticker

6/recent/ticker-posts

WAATHIRIKA WA TOPE LA MGODI WA MWADUI WAKABIDHIWA NYUMBA

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme (katikati) baada ya kukata utepe wakati akizindua na kukabidhi Mradi wa Nyumba Mbadala zilizojengwa na Kampuni ya Williamson Diamonds Limited kwa ajili ya kaya zilizoathirika na tukio la kupasuka kwa bwawa la Tope Laini lililotokea Novemba 7,2022
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akionesha picha ya nyumba za awali za wananchi na nyumba za kisasa zilizojengwa na Mgodi wa Mwadui kwa ajili ya wananchi wakati akizindua na kukabidhi Mradi wa Nyumba Mbadala kwa ajili ya kaya zilizoathirika na tukio la kupasuka kwa bwawa la Tope Laini lililotokea Novemba 7,2022

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme amezindua na kukabidhi Mradi wa Nyumba Mbadala zilizojengwa na Kampuni ya Williamson Diamonds Limited kwa ajili ya kaya zilizoathirika na tukio la kupasuka kwa bwawa la Tope Laini lililotokea Novemba 7,2022 kisha tope kwenda kwenye makazi ya watu na kuleta madhara mbalimbali.

Mhe. Mndeme amekabidhi nyumba hizo leo Ijumaa Februari 2,2024 wakati wa hafla fupi ya kukabidhi nyumba 42 kati ya 44 iliyofanyika katika Mji Mpya wa Ng’wang'holo kata ya Mwadui Lohumbo wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga.

Mhe. Mndeme ameushukuru Mgodi wa Almasi wa Mwadui kwa kutekeleza maagizo yote ya Serikali ya ulipaji fidia wananchi na leo amekabidhi nyumba 42 zilizojengwa kwa gharama ya shilingi 1,727,820,000/= kwa waathirika ambao walisalia kulipwa fidia zao kwa kujengewa nyumba.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akifurahia jambo akiwa amekaa kwenye moja ya nyumba za kisasa wakati akizindua na kukabidhi Mradi wa Nyumba Mbadala zilizojengwa na Kampuni ya Williamson Diamonds Limited kwa ajili ya kaya zilizoathirika na tukio la kupasuka kwa bwawa la Tope Laini

“Leo tunakabidhi nyumba 42 kati ya nyumba 44, nyumba mbili ujenzi bado unaendelea lakini wananchi wanne ambao walikataa kujengewa nyumba watapatiwa fedha zao ili wajenge wenyewe. Tunawashukuru Mgodi wa Mwadui kwa kutekeleza maagizo ya serikali ikiwemo kuwalipa fidia wananchi walioathirika na tope laini”,amesema Mhe. Mndeme.

“Nyumba hizi ni za kisasa, mandhari na mazingira yanapendeza sana. Naomba wananchi mzitunze nyumba hizi lakini pia hakikisheni mnapanda miti ya matunda na vivuli hapa, Mgodi wa Mwadui utaleta miti. Serikali itahakikisha pia mnaletewa huduma ya maji, umeme na kuwekewa miundombinu ya barabara. Serikali inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan inawathamini sana na imesimamia zoezi hili la ulipwaji fidia na sasa mnaishi katika nyumba bora na imara na kutoka kwenye tembe na nyumba za udongo”,ameongeza Mhe. Mndeme.

Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Mkoa wa Shinyanga amesema nyumba hizo za kisasa zilizojengwa na mgodi wa Mwadui zinatakiwa kuwa za mfano hivyo wananchi wajenge nyumba za kisasa na kuepuka nyumba duni huku akiagiza wananchi ambao bado wapo kwenye maeneo hatarishi wahamie kwenye nyumba hizo mpya zilizojengwa.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akionesha picha ya nyumba za awali za wananchi na nyumba za kisasa zilizojengwa na Mgodi wa Mwadui kwa ajili ya wananchi.

“Leo historia imeandikwa Ng’wang’holo, serikali inawatakia maisha mema kwenye makazi haya salama na bora, Asante sana Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan. Nanyi wananchi msing’ang’anie kwenye maeneo hatarishi, njooni kwenye nyumba hizi za kisasa. Tunataka wananchi waishi kwenye makazi bora",amesema Mndeme.

Mhe. Mndeme pia amewaagiza Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) wilayani Kishapu pamoja na TANESCO, kupeleka huduma za maji na umeme haraka kwenye nyumba hizo ili kuboresha maisha bora kwa wananchi hao.

Meneja wa RUWASA Wilaya ya Kishapu, Mhandisi Dickson Kamazima amesema tayari Mkandarasi wa kutekeleza mradi wa mradi katika eneo hilo amepatikana na kazi ya ujenzi wa mradi itaanza hivi karibuni.
Muonekano wa sehemu nyumba zilizojengwa na Kampuni ya Williamson Diamonds Limited kwa ajili ya kaya zilizoathirika na tukio la kupasuka kwa bwawa la Tope Laini

Akitoa taarifa ya ujenzi wa nyumba hizo, Meneja Mahusiano Mgodi wa Mwadui Bernard Mihayo,  amesema gharama za mradi huo wa kujenga nyumba 44 umefikia fedha za Kitanzania shilingi 1,727,820,000.00.

Mihayo ameishukuru serikali kwa Kuunda Kamati Maalumu ya kusimamia tukio hilo ambapo katika. hatua ya kuthamini athari ilibaini kuwa ajali hiyo iliathiri kwa namna moja au nyingine nyumba 47. Vile vile hatua hiyo ilibaini pia mwananchi mmoja aliyekuwa mpangaji katika eneo hilo alikuwa anaishi katika mazingira magumu sana na hivyo busara ilitumika kuamua ajengewe nyumba Kwa hiyo Kampuni ilitakiwa kujenga idadi ya nyumba 48.

“Mpango wa mradi wa ujenzi wa nyumba katika kushirikishwa ilikubalika kwamba kila nyumba itajengwakatika eneo ambalo mwathirika mwenyewe ataridhika. Idadi ya nyumba 44 ya 48 zilioneshwa pa kujengwa ambapo 18 zipo pamoja mji mpya kijiji cha Nh’wang’holo na zilizobakia maeneo mengine 10 Ng’wang’holo, 8 Nyenze, 4 Idukilo, 2 Mwigumbi na 2 Maganzo. Kila nyumba imesanifiwa kwa ubora wa kudumu zaidi ya nyumba iliyoathirika ambapo ina jengo la nyumba ya kuishi, jiko la nje na choo na bafu cha njev ilivyounganishwa na mfumo wa maji taka”,amesema.
Ameeleza kuwa , nyumba hizo za kuishi zipo za aina tofauti kwa kutegemea uthamini za kuanzia vyumba 3 hadi 7 ambapo kila moja ikiwa na veranda ambapo Utekelezaji wa ujenzi ulisimamiwa na Kampuni. Ujenzi ulianza tarehe 1 Agosti 2023.

Mihayo amesema vifaa vya ujenzi vilivyotumika vilivyonunuliwa ndani ya mkoa wa Shinyanga ni matofali ya saruji, paa la bati, milango ya mbao ngumu, madirisha ya ‘aluminium’ yenye ‘grill’ pamoja na vioo, dari la ‘gypsum’ na kumaliziwa kupambwa kwa kupakwa rangi na Mpaka mwisho wa mwezi Disemba 2023 nyumba 42 zilikamilika kujengwa za waathirika waliokubali kujengewa awamu ya kwanza ambapo wengi wamehamia.

“Kuanzia mwezi Januari 2024 hadi leo nyumba 2 zinaendelea kujengwa za waathirika waliokubali awamu ya pili ambapo zipo hatua ya‘lintel’ na zinategemewa kumalizika mwezi ujao. Ujenzi umefanikiwa kwa ushirikiano mzuri uliotolewa hususani na Waathirika wenyewe, Viongozi wa Serikali ngazi za Vijiji, Kata, Wilaya, Mkoa na Taasisi nyingine”,ameongeza.

“Kampuni inashauri Waathirika watunze na watumie vizuri majengo mapya na vifaa vyake na kuboresha mazingira ya maeneo yao kwa manufaa yao na vizazi vyao. Hatua inayofuata Kampuni itatekeleza mradi wa kuhamisha makaburi 14 ya baadhi ya waathirika wanaokabidhiwa nyumba ambapo taratibu za kisheria za kuhamisha zimekamilika. Pia itatekeleza miradi ya kuwaboreshea vipato ikiwemo kufuga kuku 3,600 au mbuzi 304”,amesema.

“Mhe, Mkuu wa Mkoa, Bado kuna changamoto zilizotokea. Kuna waathirika 4 wamekataa kujengewa nyumba ambapo tunaendelea na mazungumzo nao. Pia kuna baadhi ya waathirika wanaendelea kuishi katika nyumba za zamani baada ya kukabidhiwa nyumba mpya na wapo wengine wamelima maeneo waliyofidiwa licha ya Kampuni kufanya mazungumzo nao. Kampuni inawaomba waathirika kuacha kutumia maeneoyaliyoathirika kwa usalama wao”,amesema  Mihayo.

Nao baadhi ya wananchi ambao wamekabidhiwa nyumba hizo akiwemo Mihambo Salu na Hamis Bilal wameishukuru Serikali pamoja na Mgodi wa Mwadui kwa kuwajengea nyumba hizo na kuomba wapatiwe huduma za umeme na maji ili kufurahia maisha zaidi.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akizungumza  leo Ijumaa Februari 2,2024 wakati akizindua na kukabidhi Mradi wa Nyumba Mbadala zilizojengwa na Kampuni ya Williamson Diamonds Limited kwa ajili ya kaya zilizoathirika na tukio la kupasuka kwa bwawa la Tope Laini lililotokea Novemba 7,2022 - Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akiangalia picha ya nyumba za awali za wananchi na nyumba za kisasa zilizojengwa na Mgodi wa Mwadui kwa ajili ya wananchi wakati akizindua na kukabidhi Mradi wa Nyumba Mbadala kwa ajili ya kaya zilizoathirika na tukio la kupasuka kwa bwawa la Tope Laini lililotokea Novemba 7,2022
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akionesha picha ya nyumba za awali za wananchi na nyumba za kisasa zilizojengwa na Mgodi wa Mwadui kwa ajili ya wananchi wakati akizindua na kukabidhi Mradi wa Nyumba Mbadala kwa ajili ya kaya zilizoathirika na tukio la kupasuka kwa bwawa la Tope Laini lililotokea Novemba 7,2022
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme (katikati) akikata utepe wakati akizindua na kukabidhi Mradi wa Nyumba Mbadala zilizojengwa na Kampuni ya Williamson Diamonds Limited kwa ajili ya kaya zilizoathirika na tukio la kupasuka kwa bwawa la Tope Laini lililotokea Novemba 7,2022
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme (katikati) akisoma maandishi wakati akizindua na kukabidhi Mradi wa Nyumba Mbadala zilizojengwa na Kampuni ya Williamson Diamonds Limited kwa ajili ya kaya zilizoathirika na tukio la kupasuka kwa bwawa la Tope Laini lililotokea Novemba 7,2022

Maandishi katika Mradi wa Nyumba Mbadala zilizojengwa na Kampuni ya Williamson Diamonds Limited kwa ajili ya kaya zilizoathirika na tukio la kupasuka kwa bwawa la Tope Laini lililotokea Novemba 7,2022
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akikata utepe kuzindua na kukabidhi moja ya nyumba zilizojengwa na Kampuni ya Williamson Diamonds Limited kwa ajili ya kaya zilizoathirika na tukio la kupasuka kwa bwawa la Tope Laini

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akiwa katika moja ya nyumba zilizojengwa na Kampuni ya Williamson Diamonds Limited kwa ajili ya kaya zilizoathirika na tukio la kupasuka kwa bwawa la Tope Laini
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akikagua choo na bafu katika moja ya nyumba zilizojengwa na Kampuni ya Williamson Diamonds Limited kwa ajili ya kaya zilizoathirika na tukio la kupasuka kwa bwawa la Tope Laini
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akikagua  nyumba zilizojengwa na Kampuni ya Williamson Diamonds Limited kwa ajili ya kaya zilizoathirika na tukio la kupasuka kwa bwawa la Tope Laini

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akipnda mti katika Mji Mpya wa Ng'wang'holo wakati akizindua na kukabidhi Mradi wa Nyumba Mbadala zilizojengwa na Kampuni ya Williamson Diamonds Limited kwa ajili ya kaya zilizoathirika na tukio la kupasuka kwa bwawa la Tope Laini
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akipanda mti katika Mji Mpya wa Ng'wang'holo wakati akizindua na kukabidhi Mradi wa Nyumba Mbadala zilizojengwa na Kampuni ya Williamson Diamonds Limited kwa ajili ya kaya zilizoathirika na tukio la kupasuka kwa bwawa la Tope Laini
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akifurahia jambo wakati akipanda mti katika Mji Mpya wa Ng'wang'holo wakati akizindua na kukabidhi Mradi wa Nyumba Mbadala zilizojengwa na Kampuni ya Williamson Diamonds Limited kwa ajili ya kaya zilizoathirika na tukio la kupasuka kwa bwawa la Tope Laini
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akizungumza na wananchi akiwa amekaa kwenye moja ya nyumba wakati akizindua na kukabidhi Mradi wa Nyumba Mbadala zilizojengwa na Kampuni ya Williamson Diamonds Limited kwa ajili ya kaya zilizoathirika na tukio la kupasuka kwa bwawa la Tope Laini

Wananchi wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme
Wananchi wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Modest Mkude akizungumza katika eneo Mradi wa Nyumba Mbadala zilizojengwa na Kampuni ya Williamson Diamonds Limited kwa ajili ya kaya zilizoathirika na tukio la kupasuka kwa bwawa la Tope Laini
Meneja Mahusiano Mgodi wa Mwadui Bernard Mihayo akisoma taarifa ya Mradi wa Nyumba Mbadala zilizojengwa na Kampuni ya Williamson Diamonds Limited kwa ajili ya kaya zilizoathirika na tukio la kupasuka kwa bwawa la Tope Laini 

Meneja wa RUWASA Wilaya ya Kishapu, Mhandisi Dickson Kamazima akielezea namna watakavyopeleka maji kwenye nyumba hizo
Diwani wa kata ya Mwadui Luhumbo Mhe. Francis Manyanda akizungumza wakati wa hafla hiyo
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kishapu, Shija Ntelezu akizungumza wakati wa hafla hiyo

Mmoja wa wananchi akiishukuru serikali na Mgodi wa Mwadui kujenga nyumba za kisasa na kulipa fidia wananchi

Picha za kumbukumbu
Picha za kumbukumbu
Picha za kumbukumbu

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Post a Comment

0 Comments